Tetesi za soka Ulaya Jumatano 11.03.2020: Lacazette, Werner, Mbappe, Bellingham, Sidibe, Doku, Pochettino

Mauricio Pochettino
Image captionAliyekuwa mkufunzi wa Tottenham Maurico Pochettino
Real Madrid huenda ikamtimua kocha wake Zinedine Zidane na kumuajiri aliyekuwa kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ama aliyekuwa kocha wa Juventus Massimiliano Allegri.(Marca - in Spanish)
Atletico Madrid inasalia na nia kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre lacazette ,28, kutoka Arsenal. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barcelona imemweka mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 24, kama chaguo la pili nyuma ya mshambuliaji wa Inter Milan na Lautaro Martinez, 22. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Timo warner
Image captionMshambuliaji wa RB Leipzig Timo Warner
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, alifanyiwa vipimo vya corona kabla ya mechi ya klabu bingwa kati ya Paris-St Germain dhidi ya Borussia Dortmund - na kuonekana hana maambukizi ya ugonjwa huo. (L'Equipe - in French)
Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson anajaribu kuisaidia klabu hiyo kumsaini Jude Bellingham kutoka Birmingham baada ya kukutana na wazazi wa kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 16 wakati walipotembelea uwanja wa mazoezi wa Old Trafford siku ya Jumatatu(Star)
Beki wa Monaco na Ufaransa Djibril Sidibe, 27, anasema kwamba anataka mkataba wake katika klabu ya Everton kuwa wa kudumu. (RMC Sport, via Liverpool Echo)
Djibril Sidibe
Image captionBeki wa Monaco na Ufaransa Djibril sidibe anataka kuimarisha mkataba wake na Everton
Liverpool inatumaini kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Jeremy Doku, 17, baada ya uhamisho wa awali wa kinda huyo kugonga mwamba. (Het Nieuwsblad, via Star)
Wakala Mino Raiola anasema kwamba mawakala wengine wakuu wanaunga mkono mipango mingine ya mfumo mbadala wa uhamisho ambao unaweza kuiharibu Fifa vibaya.. (Telegraph - subscription required)
Uefa inafikiria kuahirisha michuano ya Euro 2020 kwa mwaka mmoja kutokana na mlipuko wa virusi vya corona kufuatia maombi yaliowasilishwa na mashirika tofauti ya soka duniani. (Tuttosport - in Italian)
Mino Raiola
Image captionWakala maarufu Mino Raiola
Wakala Jorge Alvial aliwasilisha ripoti 40 katika klabu ya Manchester United kuhusu uhamisho wa Alphonso Davies - kabla ya Bayern Munich kumsaini winga huyo wa Canada , 19, kutoka Vancouver Whitecaps. (Sun)
Arsenal inajaribu kuimarisha hatma ya winga wa England Bukayo Saka, 18, huku Man United wakivutiwa na mchezaji huyo. (Express)

TETESI ZA SOKA JUMANNE

Jack GrealishHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiungo mshambuliaji wa Asto Villa Jack Grealish ananyatiwa na Man United
Manchester United inapanga uhamisho wa dau la £100m kumsajili kiungo wa kati wa Aston Villa mwisho wa msimu huu Jack Grealish, 24, na kinda wa Birmingham 16- Jude Bellingham. (Star)
Kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 27,anatarajiwa kuuzwa na Man United mwisho wa msimu huu . (Goal)
Winga wa Chelsea na Brazil Willian, 31, amekiri kwamba hajui pale ambapo hatma yake ipo , huku kandarasi yake ikitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu huku mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakikwama. (Evening Standard)
WillianHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionmchezaji wa Brazil na Chelsea Willian
Mkewe Willian Vanessa Martins amependekeza kwamba mumewe huenda anakaribia kukamilisha kipindi chake cha miaka saba akiichezea timu hiyo.. (Mirror)
Manchester United inaongoza ushindani wa kumsajili beki wa Borussia Monchengladbach na Switzerland Denis Zakaria, 23. (Star)
Manchester City ina matumaini kwamba mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 31, ambaye ndiye mfungaji wa mabao mengi hatawasilisha ombi la kutaka kuhamia klabu nyengine mwisho wa msimu huu , licha ya kwamba klabu hiyo huenda ikakabiliwa na marufuku ya kushiriki mechi za klabu bingwa Ulaya. (Evening Standard)
Sergio AgueroHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJe Sergio Aguero atataka kuhamia klabu nynegine wakatia mbapo huenda Manchester City ikakabiliwa na marufuku ya kushiriki kombe la klabu bingwa?
Barcelona inataka kumpatia kandarasi mpya kiungo wa kati wa Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 27, na wana imani kufanya hivyo licha ya kuvutia hamu kutoka timu nyengine ikiwemo Chelsea. (Sport)
Aliyekuwa bingwa wa ndondi katika uzani wa kati Floyd Mayweather amesema kwamba anataka kuinunua klabu ya Newcastle. (Newcastle Chronicle)
Inter Milan huenda ikamnunua kipa wa Bosnia na Bournemouth Asmir Begovic, 32, ambaye kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya AC Milan, kuwa naibu wa kipa wa Slovenia Samir Handanovic, 35, msimu ujao. (La Repubblica, via Sempre Inter)
Kipa wa Real Madrid na Ubelgiji Thibaut Courtois 27, huenda asishiriki mechi nyingi na klabu hiyo msimu ujao na hata zile za kombe la klabu bingwa dhidi ya Manchester City kutokana na jeraha analouguza katika mguu wake wa kushoto. (ESPN)
Thibaut CourtoisHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKipa wa Real Madrid Thibaut Courtois anaguzua jeraha la mguu wake wa kushoto
Leeds imejiunga na Southampton katika onyo la kutaka kumsaini beki wa Oxford na England Rob Dickie, 24. (Football Insider)
Arsenal bado inamnyatia beki wa kushoto wa Ufaransa na Paris St-German Layvin Kurzawa, 27. (France Football, via Sport Witness)
Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Ujerumani Emre Can, 26, amefichua kwamba alikataa ofa kutoka klabu tatu za ligi ya England ikiwemo Manchester United, kwa kuitii klabu yake ya zamani (Mail)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26,
Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26, alimwabia wakala wake kufutilia mbali uhamisho wake kuelekea Manchester United - wakati mwakilishi wa mchezaji huyo alipokuwa katika ofisi ya afisa mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward. (Calciomercato, via Mirror)
Real Madrid inafikiria kumsajili kipa wa Chelsea na Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, mwisho wa msimu huu, huku the Blues ikiwa na hamu ya kuwanunua makipa wawili kwa mkopo Marc-Andre Ter Stegen na mwenzake wa Manchester United na England Dean Henderson, 22. (Star)
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anapanga kumpatia kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 28, mkataba mpya wa mshahara wa £350,000 kwa wiki. (Express)
Kevin De Bryune
Image captionKevin De Bryune
Mlinda mlango wa England Dean Henderson, 22, amemwambia mwenzake wa Sheffield United atarudi kwa mkopo katika klabu hiyo msimu ujao iwapo hataanzishwa katika klabu ya Manchester United. (Mail)
Arsenal huenda ikamuwania mchezaji wake wa zamani wa timu ya vijana Donyell Malen aliyeondokja Arsenal na kujiunga na klabu ya PSV mwaka 2017. (Le10Sport)
Kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher, 20, aliye kwa ,mkopo katika klabu ya Swansea, ananyatiwa na klabu ya Uholanzi Vitesse Arnhem kwa usajili wa mkopo. (Sun)
Manchester United wana matumaini wanaweza kumshawishi winga wa Uholanzi Tahith Chong mwenye umri wa miaka 20 kusalia katika klabu hiyo , licha ya klabu ya Barcelona , Inter na Juventus kuonesha
nia naye. (Sun)
Tahith ChongHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTahith Chong
Tottenham inafikiria kumsajili beki wa kushoto mwisho wa msimu huu na wamemlenga mchezaji anayedaiwa kuwa na thamani ya £22m Borna Barisic, 27 , raia wa Croatia ambaye kwa sasa anaichezea Rangers. (90 Min)
Kocha wa Manchester Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba Manchester United inahitaji wachezaji wawili ama watatu wapya ili kuonekana kama washindani wa taji la ligi ya Uingereza licha ya kuilaza Manchester City nyumbani na ugenini msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 10 (ESPN)
Mshambuliaji wa Ufaransa na Chelsea Olivier Giroud, 33, amefichua kwamba alizuiliwa kujiunga na Tottenham katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (90 Min)
Olivier Giroud
Image captionMshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud
Giroud amekiri alikuwa na hamu ya kujiunga na Inter wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari (Calciomercato)
Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ambaye anaendelea kuhusishwa na uhamisho amesisitiza kuwa anafurahia kusalia Arsenal. (Mirror)
Chelsea inaongoza ushindani wa kutaka kumsajili mchezaji wa klabu ya Aldershot na England ,17, Reece Wylie. (Team Talk)
Winga wa Bournemouth na Wales Harry Wilson, 22, anayecheza kwa mkopo Liverpool , alipigwa picha akiwa amevalia koti jekundu katika mkutano huo wa klabu hizo mbili siku ya Jumamosi lakini akasisitiza kwamba alipatiwa na mfanyakazi wa Liverpool kwa sababu kulikuwa baridi.. (Liverpool Echo)
Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang
Liverpool huenda ikapewa fedha mwisho wa msimu huu kufuatia kifungo cha sheria cha asilimia 30 alichowekewa mchezaji wa Uhispania Luis Alberto, 27, kwenda Lazio na mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Michael Edwards. (Star)

Post a Comment

0 Comments