India: Wanaume wanne wanyongwa kwa kumbaka mwanamke ndani ya basi

Wanaume wanne wabakaji (kutoka kulia hadi kushoto ): Vinay, Pawan, Mukesh, AkshayHaki miliki ya pichaDELHI POLICE
Image captionWanaume hao wanne walikanusha mashitaka
Wanaume wanne raia wa India waliofungwa kwa kumbaka na kumuua na mwanafunzi mjini Delhi mwaka 2012 wamenyongwa.
Akshay Thakur, Vinay Sharma, Pawan Gupta na Mukesh Singh walihukumiwa kifo na mahakamani mwaka 2013.
Wanne hao walinyongwa katika gereza kuu la Tihar ikiwa ni mara ya kwanza hukumu ya kifo kutekelezwa India kutoka mwaka 2015.
Muathiriwa alifariki kutokana na majeraha aliyopata siku kadhaa baada ya kubakwa na wanaume sita ndani ya basi.
Kisa hicho kilizua ghadhabu ya umma ambayo ilichangia kubuniwa kwa sheria mpya dhidi ya ubakaji nchini India.
Mwanafunzi huyo wa miaka 23-aliyepewa jina la Nirbhaya -na vyombo vya habari kuashiria mjasiri - hakuweza kutajwa jina lake halisi kwa mujibu wa sheria za India.
Watu sita walikamatwa kwa kumshambulia. Mmoja wao, Ram Singh, alipatikana akiwa amefariki ndani ya jela mwezi Machi mwaka 2013, katika kile kinasadikiwa kuwa tukio la kujitoa uhai.
Kulingana na sheria za India mhalifu ambaye hajatimiza miaka 18 hufichwa suraHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKulingana na sheria za India mhalifu ambaye hajatimiza miaka 18 hufichwa sura
Mwingine ambaye aliyekuwa na miaka 17 wakati wa shambulio hilo, aliachiliwa huru mwaka 2015 baada ya kufungwa kwa miaka mitatu katika kituo cha kurekebisha tabia - muda ambao ni wa mwisho kumfunga mtoto nchini.
Katika miezi ya hivi karibuni, wafungwa wote wanne waliwasilisha ombi katika mahakama ya juu zaidi katika juhudi ya kutaka hukumu yao ibadilishwe kutoka kua kifo hadi kifungo cha maisha gerezani.
Lakini ombi lao lilikataliwa hatua ambayo iliwaacha bila njia nyingine ya kisheria ya kujinusuru. Rufaa ya mwisho ya kutaka hukumu ya kifo isitekelezwe dhidi yao pia ilikataliwa saa kadhaa kabya ya wote wanne kunyongwa.
Dakika kadhaa baada ya wafungwa hao kunyongwa Ijumaa asubuhi, mama yake muathiriwa alisema, "Nilitundika picha ya binti yangu ukutani na kumwambia hatimaye tumepata haki."
Baba yake alisema "Mahakama imerejesha hadhi yake".
An anti-rape protest in IndiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Usalama ulikuwa umeimarishwa nje ya jela walikonyongewa wabakaji hao huku maafisa wa polisi wakipelewa kudumisha sheria.
Kundi la watu waliokuwa wamekusanyika nje ya lango la gereza hilo wakiwa wamebeba mabango walianza kusherehekea baada ya tangazo la kunyongwa kwa wafungwa hao wanne kutolewa.
Baadhi ya waliimba "kifo kwa wabakaji" na huku wakishukuru idara ya mahakama kwa haua hiyo.
Nini kilimkuta Nirbhaya?
Mwanafunzi huyo alipanda basi karibu saa mbili na nusu za usiku Disemba 16, 2012 akiwa na rafiki wa kiume. Walikuwa wanarejea nyumbani baada ya kutizama filamu katika ukumbi wa sinema.
Wanaume sita ambao walikuwa ndani ya basi hilo, waliwashambulia ni na kisha kuanza kumbaka kwa zamu mwanamke huyo na baada ye kuanza kumpiga kwa kutumia kifaaa butu. Rafiki yake pia alipigwa.
Polisi wakikagua basi ambalo mwanafuzi alibakwa ndaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPolisi wakikagua basi ambalo mwanafuzi alibakwa ndani
Baada ya hapo walirushwa nje ya basi na kuachwa wafe. Wapita njia waliowapata waathiriwa wakiwa uchi na nyuso zilizojaa damu waliifahamisha polisi.
Wiki mbili baadae - maandamano ya umma ya kushinikiza India kuingilia kati jinsi inavyoshughulikia masuala ya wanawake. Muathiriwa alifariki katika hospitali moja nchini Singapore, ambako alipelekwa kwa matibabu baada ya hali yake kuzorota katika hospitali ya Delhi.

Post a Comment

0 Comments