Coronavirus: Waziri wa afya Uingereza Nadine Dorries akutwa na maambukizi


Nadine Dorries
Image captionNadine Dorries

Waziri wa afya na mbunge wa chama cha Conservative nchini Uingereza Nadine Dorries amesema amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Bi Dorries, mbunge wa kwanza kugundulika na maambukizi, alichukua tahadhari zote baada ya kubaini kuwa ameathirika, na amejiweka karantini nyumbani kwake.
Hali hii imekuja wakati kukiwa na taarifa ya kifo cha mtu wa sita kutokana na virusi vya corona nchini Uingereza ambako kuna visa vya watu 382 kuambukizwa.
Mtu aliyepoteza maisha hivi karibuni ni mzee mwenye umri wa miaka 80 ambaye alikuwa na changamoto za kiafya.
Wakati huohuo hospitali kuu Uingereza imesema inaboresha uwezo wake wa kuwapima watu, wakati idadi ya maambukizi ikitegemewa kuongezeka.
Hii itamaanisha kuwa vipimo 10,000 kwa siku vinaweza kufanywa- kwa saa watu 1,500 hupimwa kwa siku.
Pia kuhakikisha kuwa majibu ya vipimo yanatolewa mapema ndani ya saa 24.

Bango lenye ujumbe kuhusu coronaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBango lenye ujumbe kuhusu corona

Bi Dorries, mbunge wa Bedfordshire ya kati, amesema katika taarifa yake kuwa Idara ya afya imeanza kuwafuatilia watu waliokuwa karibu naye, na ofisi yake ya bunge inafuatilia hilo kwa karibu.
Alieleza kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu hali aliyokuwa nayo, lakini akielezea hofu aliyonayo kuhusu mama yake ,84, anayeishi naye ambaye naye ameanza kukohoa siku ya Jumanne.
Haijulikani ni vikao vingapi Bi Dorries amehudhuria Westminster au katika jimbo lake hivi karibuni.
Idara ya afya imesema alianza kuonesha dalili siku ya Alhamisi juma lililopita -alipohudhuria dhifa iliyofanyika Downing Street iliyohodhiwa na Waziri Mkuu Boris Johnson- na akawekwa karantini tangu siku ya Ijumaa.
No 10 hajatoa taarifa yoyote kama Waziri Boris Johnson amefanya vipimo vyovyote, au atapimwa sasa.
Mawaziri wote wa afya, akiwemo Waziri Mkuu wa afya Matt Hancock, watafanya vipimo, sambamba na maafisa wengine ambao walikaribiana na bi Dorries.
Bwana Hancock aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa ''amefanya jambo sahihi'' kwa kujitenga nyumbani na ''namtakia afya njema''.
Aliongeza: ''Ninaelewa kwanini watu wana wasiwasi kuhusu ugonjwa huu. Tutafanya vyovyote tunavyoweza kuwaweka watu katika hali ya usalama.

Watu wanaweza kuombwa wabaki nyumbani kwa muda wa wiki mbili kama walikuwa karibu na watu wenye maambukizi ya virusi vya coronaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu wanaweza kuombwa wabaki nyumbani kwa muda wa wiki mbili kama walikuwa karibu na watu wenye maambukizi ya virusi vya corona

Idadi ya watu walioambukizwa nchini Uingereza ni 324 England, 27 Scotland, 16 Ireland Kaskazini na 15 Wales.
Watu 91 jijini London, huku Kusini-Mashariki, kukiwa na visa 51.
Ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza imewataka raia kufanya safari zilizo muhimu pekee kwenda Italia, ambayo ina maambukizi makubwa zaidi baada ya China.
Raia wa Italia wameamriwa kubaki nyumbani, na kuomba ruhusa kwa safari muhimu.
Idara ya mambo ya nje imeshauri kuwa mtu yeyote anayewasili Uingereza kutokea Italia tangu siku ya Jumatatu, ajiweke karantini kwa siku 14.
Serikali imesema inaweza kutoa msaada wa eneo la karantini kwa raia wa Italia watakaokuwa wanajiweka karantini.
Shirika la ndege la Uingereza limeahirisha safari za kwenda na kutoka Italia mpaka tarehe 4 mwezi Aprili, na limewataka wafanyakazi kujitolea kwenda likizo bila malipo.

Post a Comment

0 Comments