Hamu ya raia wa mataifa mengi ya magharibi ya kuvalia mavazi yenye mitindo ya kisasa imepelekea kuwepo kwa nguoza ziada ndani ya kabati za familia nyingi.
Nguo hizo ambazo hazitumiki mara nyingi hupeanwa kwa marafiki na mashirika yasio ya kiserikali kama vile Oxfam na mengineyo.
Mtindo huu umeimarika haswa kufwatia kuongezeka kwa nguo za bei nafuu kutoka mataifa ya mashariki ya mbali na China kwa kiwango kikubwa.
Hapo kulingana na mtafiti Daktari Andrew Brooks wa chuo kikuu cha Kings College ndipo nguo hizo zinageuka na kuwa bidhaa muhimu.
Nguo kuukuu au mitumba ni za bei nafuu hususan kwa walala hoi katika mataifa mengi ya Afrika.
Mbali na kuwa ni za bei na fuu wanaozipenda hudai kuwa vitambaa vyake ni vya viwango vya juu kuliko vile vinavyotengezwa hapa nchini.
Hii ni kwa saababu nguo hizo hutoka nje ya nchi kama vile Ulaya na Marekani.
Marekani imejijengea sifa ya kuwa taifa linalofaidika zaidi kutokana na biashara hii ya nguo kuukuu.
Kulingana na takwimu za umoja wa mataifa Taifa hilo linazoa takriban dola milioni 687 kila mwaka .
TanzaniUingereza ni ya pili,ikijizolea zaidi ya dola milioni 600 kutoka kwa wanunuzi wa nguo hizo.
Ajabu ni kwamba Uingereza iliuza nguo tani 351,000 mwaka wa 2013 .
Nguo hizo zinavaliwa sasa nchini Poland, Ghana, Pakistan na Ukraine.
Nguo zinazovaliwa marekani zinauzwa Canada, Chile, Guatemala na India.
Biashara ya mitumba katika miji mikuu imeshamiri na huenda ikawa ndio kitovu cha biashara katika eneo la Afrika Mashariki.
Mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango ametembelea soko la Owino ambalo inasemekana sio tu soko kubwa katika kanda ya Afrika mashariki na kati lakini sehemu kubwa ya soko hilo inashughulikia nguo kuukuu.
Soko la Owino lililoko Kampala linasemekana ndilo kubwa zaidi katika eneo la Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa maafisa wa soko hili, lina wachuuzi zaidi ya elfu mbili wanaofanya mahali hapo kila siku na hupokea wateja zaidi ya millioni moja kwasiku.
Kuna wanaouza nguo hizo chini ya vyumba ilhali wengine huweka bidhaa zao chini na inakuwa kazi kubwa kuweza kuwashawishi wateja kuja katika kibanda chake kuweza kununua ndio maana baadhi ya vijana wakaamua kufanya vitu vyao
Suala la kununua nguo za ndani mitumba pia limewashangaza wengi wakiona kinyaa kununua chupi mtumba.
Mbali na hayo ,ubora wa mitumba pamoja na bei yake nafuu na kutoa ajira pia kuna jambo lingine kwa wale wanaojihusisha na biashara hiyo-yaani- hujipatia donge nono.
Kuna wanaopata dola 200 kwa siku kutokana na biashara hii .
Ni juzi tu kulitolewa ripoti ikigusia kushamiri kwa biashara ya mitumba katika eneo la Afrika mashariki na kati.
Kwa mujibu wa mtafiti Andrew Brooks madhara ya ufanisi wa biashara hii kwa chumi za mataifa husika ni kubwa sana.
Kwa mfano tangu miaka ya Themanini na Tisini biashara hii imepunguza utashi wa nguo mpya katika mataifa kama vile Kenya, Malawi, Mozambique, Nigeria, Rwanda, Senegal, Swaziland, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.
Uganda ambayo awali ilikuwa na viwanda tele vya nguo sasa inategemea nguo kuukuu kwa asilimia 81 %
Si hayo tu Bwana Brooks anasema kuwa Ghana ilipoteza nafasi asilimia 80% za ajira katika sekta ya nguo kati ya mwaka wa 1975 na 2000.
Nigeria kwa upande wake ilipoteza nafasi 200,000 za kazi kufuatia kushamiri kwa nguo kuu kuu.
0 Comments