Ezzeldin Bahader: Mwanasoka mkongwe duniani aliyefunga bao akiwa na miaka 75

Ezzeldin BahaderHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionEzzeldin Bahader ni mchezi mpira mkongwe anayelipwa
Mchezaji mpira mkongwe anayelipwa ambaye ni raia wa Misri ameweza kupata goli kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 75.
Ezzeldin Bahader anapaswa kucheza michezo miwili kila mchezo akiwepo dakika tisini zote ndio atakuwa anastaili kuingia katika kitabu cha kihistoria cha waliovunja rekodi 'Guinness World Records book'.
Alianza kwa mtindo wa kuvutia , alicheza kwa dakika 90 licha ya kuumia siku ya jumamosi katika timu ya 6 Oktoba, ya soka la wamisri.
Mchezaji huyu ambaye ni baba wa watoto wanne na babu wajukuu sita aliweza kufunga kwa penati wakati aliposukumwa na wachezaji wenzakati na kufanya timu yake itoke na matokeo ya 1-1.
"Nimetambuliwa kuwa mchezaji mkongwe wa kulipwa baada ya kufunga goli katika mechi rasmi ," alisema.
"Hiki ni kitu ambacho nilifanikiwa kukipata katika dakika za mwisho wa mchezo, nilikuwa sitarajii kufanikiwa katika hili kabisa. Niliumia na nilichokuwa natamani ni kumaliza dakika 90 na kucheza mechi nyingine."
Baada ya mechi, vijana walimtafuta bwana Bahader ili wapige naye picha wakiwa na wachezaji waliofungwa.
Isaak Hayik mchezaji soka mkongwe dunianiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionIsaak Hayik mchezaji soka mkongwe duniani
Lazima acheze mchezo mwingine kwa dakika 90 zote, mechi nyingine inatarajiwa kuchezwa tarehe 21 Machi ambapo anaweza kutambuliwa rasmi kuwa ndiye mchezaji mzee zaidi duniani katika kitabu cha Guinness World Records.
Ezzeldin Bahader ni nani?
Rikodi ya dunia ya sasa inamtambua Muisrael Isaak Hayik mwenye umri wa miaka 73 na dakika 95 kuwa mchezaji mzee zaidi duniani, baada ya kucheza na kufunga mwaka jana katika mechi dhidi ya Israeli na Ironi au Yehuda.
Mshambuliaji huyo hivi karibuni amekuwa na jeraha katika goti, aikuwa anacheza mpira huku akiwa anafanya shughuli zake za kutoa ushauri katika uhandisi na mtaalamu wa masuala ya ardhi.
Mwezi Januari, shirikisho la soka nchini Misri lilimsajiri mchezaji huyo ambapo hapo awali alikuwa haonekani kuwa mchezaji wa kulipwa kwa taaluma yake.
Alianza kucheza mpira mtaani katika mji mkuu wa Misri, Cairo akiwa na umri wa miaka sita, ni baada ya miongo saba ndio ameweza kusajiliwa katika klabu na kufanikisha ndoto zake.
Isaak Hayik, the world's oldest football player, seen playing for his team Ironi Or YehudaHaki miliki ya pichaREUTERS
Klabu iliyoko mjini Cairo-October 6 ndio klabu iliyomsajiri na ikiwa na jicho la kumuingiza katika kitabu cha kuvunja rekodi.
"Ili ni jambo jema kwa Misri kuwa na mtu katika kitabu cha kuvunja rekodi 'Guinness Book of Records' na kuwa naye katika klabu ya October 6 ," alisema kocha wake Ahmed Abdel Ghany.
"Kiukweli , hatutafaidika na chochote kutoka kwake kwa 100% lakini tunaweza kumfanya imara acheze dakika 90 au 180 (ili kuwa na vigezo vya kuingia katika kitabu cha Guinness World Records book)."
Bahader amekuwa akipewa mafunzo katika klabu hiyo na akiwa nyumbani pia amekuwa na kocha wake binafsi.

Post a Comment

0 Comments