Coronavirus: Jinsi wahalifu wa mtandaoni wanavyoongeza hofu katika jamii

Envelope with virusHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wataalamu wa masuala ya usalama wamesema kuwa, mlipuko wa virusi vya corona umefanya wahalifu wa mtandaoni kutumia mwanya huu kutapeli watu pia.
Wahalifu wa mtandaoni wanawalenga watu binafsi pamoja na sekta mbalimbali kama usafiri, utalii,afya ,elimu, bima na shughuli nyingine.
Barua pepe za ulaghai ambazo zinaandikwa kwa lugha ya kiingereza, kifaransa, kiitaliano, kijapani na kituruki zimebanika.
BBC imefuatilia barua hizo.
1. Kuna barua ambazo zinaelekeza wapi watu wanaweza kupata tiba ya corona
Email scam screenshotHaki miliki ya pichaPROOFPOINT
Image captionMuathirika akiwa anatafuta tiba akuta taarifa zake zimeibiwa
Watafiti katika makosa ya kihalifu wamethibitisha kuwa walligundua barua pepe ambayo hawakuielewa kutoka kwa wateja mwezi Februari.
Ujumbe ukiwa umetoka kwa daktari anayedai kuwa kuna chanjo ambayo imebainika iliyotengenezwa na serikali ya China na Uingereza.
Inawataka watu kufungua nyaraka hiyo ambayo ina maelezo kuhusu chanjo.
Barua pepe zipatazo 200,000 zimetumwa kwa wakati mmoja kwa watu tofauti.
"Tumeona mawasiliano mengi kwa siku kadhaa ambazo zinafanya kampeni kuhusu corona ambayo haieleweki, wengi wakiwa wanawaogopesha watu ili kuwashawishi wafungue nyaraka hiyo." alisema Sherrod DeGrippo kutoka katika kampuni ambayo inafanya utafiti wa vitisho hivyo vya mtandao.
Utafiti unasema kuwa utapeli huo unafanyika kila siku.
Ukweli ni kwamba kampeni hizi za uhalifu mtandaoni zinapata mapokeo yaliyogawanyika.
Cha muhimu tu ni kwamba watu wasifungue nyaraka hizo ambazo zinazunguka mitandaoni kuwatapeli.
2. Kodi kwa ajili ya Covid-19
Screenshot of email tax scamHaki miliki ya pichaMIMECAST
Watafiti wa makosa ya kimtandao wamewakamata baadhi ndani ya wiki kadhaa.
Lakini kwa mfano asubuhi tu ya leo, zaidi ya walaghai wa mtandaoni 200 wameonekana kwa muda mfupi tu.
Kama mtu akibonyeza kitufe cha nyaraka cha yeye kupata ufadhili kutoka katika serikali ya uongo na huku wakihamasisha watu kutoa kodi na kupokea taarifa za kodi.
Jambo la muhimu ni kutojibu barua pepe hizo, kwa kuwa hao ni wezi.
3. Hatua ndogo za kukabiliana na corona
Screenshot of fake WHO scamHaki miliki ya pichaPROOFPOINT
Image captionWahalifu wa mtandaoni wameamua kutumia jina la shirika la afya duniani
Kuna wahalifu wa mtandaoni wanadai kuwa wanawakilisha shirika la afya duniani (WHO) na kueleza namna gani wanaweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.
"Ukichukua hatua hii utapona,"hayo ndio madai yao.
Lakini watafiti wanasema kuwa ushauri amabao wanautoa huwa hauna msaada wowote zaidi ya kuathiri komputa yako kwa kuweka programu ijulikanayo kama
'AgentTesla Keylogger'.
Rekodi hiyo inawasaidia waweze kufuatilia waathirika wao katika mtandao.
Kuzuia uhalifu huu ambao unadai unatoka WHO, wakati ni feki.
Ni vyema watu kutembelea tovuti rasmi ya WHO au kurasa zao za mitandao.
4. Virusi vinavyoambukizwa kwa njia ya hewa
Screenshot of fear-inducing email scamHaki miliki ya pichaCOFENSE
Wahalifu wngine wa mitandaoni wanadai kuwa Covid-19 ni magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa na hivyo kufanya maambukizi kusambaa zaidi katika jumuiya .
Barua hiyo imeandikwa kama vile imetoka katika kituo cha kukabiliana na magonjwa (CDC).
Wahalifu wa mtandao wanadaiwa kutumia njia hiyo hili kuwatisha watu.
Lakini njia nzuri ya kujilinda na barua pepe za namna hiyo ni kuhakiki.
5. Changia hapa ili kukabiliana na mapambano
Screenshot of CDC Bitcoin scamHaki miliki ya pichaKASPERSKY
Hakuna ukweli kuwa kituo cha kukabiliana na magonjwa kinatafuta michango.
Barua pepe feki ambazo zinawataka watu kuchangia ili chanjo iweze kutengenezwa ni utapeli tu.
Zaidi ya barua pepe 513 zimeeleza kuhusu virusi vya corona vinasababisha kushambuliwa kwa komputa na malware.


    "Tunategemea kuwa tatizo linakuwa siku baada ya siku, wakati virusi kweli vikiendelea kusambaa lakini usalama wa mtandaoni unapaswa kuzingatiwa na kila mmoja.

    Post a Comment

    0 Comments