Zaidi ya watu 1,700 wamekwama kwenye meli ya kitalii na meli ya kubeba mizigo kwenye pwani ya Cape Town nchini Afrika Kusini kwa hofu kwamba baadhi yao wameambukizwa na virusi vya corona.
Wasiwasi uliibuka kwa mamlaka za bandari baada ya mfanyakazi wa meli ya mizigo, ambaye alikuwa safarini kutoka Uturuki mnamo 9 Machi, alipoanza kuonesha dalili za virusi.
Ametengwa kwenye meli MV Corona sambamba na mfanyakazi mwenzake ambaye alikuwa naye kwenye ndege na kutoka Uturuki
Ufuatiliaji wa mawasiliano umebaini kuwa watu wengine sita waliokuwa kwenye ndege hiyo baadae walienda kwenye walienda kwenye meli ya kifahari ya Aidamira.
Ilianza safari siku iliyofuata, ikitembelea Lüderitz na Walvis Bay huko Namibia kabla ya kurudi Cape Town hivi karibuni.
Vyombo hivyo vya majini hubeba raia wa Ujerumani na Australia.
Mamlaka za afya sasa zinasubiri majibu ya watu saba waliokaribiana na mfanyakazi wa meli ya MV Corona aliyekuwa mgonjwa. Wote wamepimwa.
''Suala la upimaji ni la lazima,'' msemaji wa wizara ya afya Popo Maja aliiambia BBC.
Afrika Kusini imethibitisha kuwa na watu 116 walioambukizwa, wengi wao watu waliohusishwana safari za Ulaya.
Hata hivyo, nchi hiyo imeanza kurekodi maambukizi miongoni mwa raia wa Afrika Kusini.
0 Comments