Rais Museveni atangaza kufunga taasisi za elimu, mikusanyiko nchini Uganda
Museveni amezuia raia wa Uganda kusafiri kuelekea kwenye nchi zilizo na maambukizi ya virusi vya corona.
Raia wa Uganda wanaowasili kutoka nje watatakiwa kujiweka karantini kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe.
Museveni ameamuru kufungwa kwa shule za msingi, sekondari na taasisi za elimu ya juu kuanzia Ijumaa tarehe 20 mwezi Machi,kwa muda wa mwezi mmoja.
Nyumba zote za ibada zimeamriwa kuahirisha mikusanyiko kwa mwezi mmoja kuanzia hivi sasa.
Mikusanyiko ya umma ikiwemo mikutano, mikutano ya kuhusu uchaguzi, mikutano ya kawaida, ya kitamaduni pia imepigwa marufuku kwa muda wa mwezi mmoja.
Hakuna taarifa ya kuwa na mtu mwenye maambukizi nchini Uganda
0 Comments