Watu 10 wa asili ya Afrika walio tajiri zaidi duniani

Dangote anaorodheshwa kuwa mtu tajiri zaidi AfrikaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionDangote anaorodheshwa kuwa mtu tajiri zaidi Afrika
Bwanyenye kutoka Nigeria Aliko Dangote ndiye mtu mweusi aliye tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Kati ya watu 2,043 ambao wameorodheshwa kuwa mabilionea duniani katika orodha ya Forbes yam waka huu, ni watu 10 pekee ambao ni weusi.
Dangote amehifadhi taji la kuwa mtu mweusi tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa takriban $14.1 bilioni.
Anafuatiwa na Mnigeria mwenzake Mike Adenuga ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa $5.3 bilioni.
Tajiri anayejihusisha na ujenzi ambaye ana uraia wa Saudi Arabia na Ethiopia Mohammed Al-Amoudi ambaye alikuwa na utajiri wa $8.4 bilioni aliondolewa kwenye orodha hiyo mwaka huu baada ya Forbes kuamua kuwaondoa mabilionea kutoka Saudi Arabia kwenye orodha yam waka huu.
Raia wa Zimbabwe aliyewekeza katika sekta ya mawasiliano, na ambaye hutoa pesa nyingi kwa hisani, Strive Masiyiwa, amejiunga na orodha ya watu weusi walio mabilionea.
Ndiye mtu wa kwanza kutoka Zimbabwe kuwa bilionea.
Binti wa aliyekuwa rais wa Angola, Isabel dos Santos, Mmarekani anayejihusisha na vyombo vya habari Oprah Winfrey na tajiri wa mafuta kutoka Nigeria Folorunsho Alakija bado ndio wanawake pekee weusi kwenye orodha ya mabilionea duniani, kwa mujibu wa jarida hilo.
Marekani ndiyo nchi iliyo na mabilionea wengi duniani, ambapo ina mabilionea 585, ikifuatwa na China. Jimbo la California pekee lina mabilionea 144, zaidi kushinda mataifa yote isipokuwa Marekani na China.
Ujerumani ndiyo nchi inayoongoza Ulaya ikiwa na mabilionea 123.
India ina mabilionea 119 nayo Urusi mabilionea 102.
Kuna mabilionea 53 kutoka Uingereza kwa mujibu wa Forbes na idadi hiyo imeshuka kutoka 54 mwaka 2017.
Presentational grey line
1. Aliko Dangote, $14.1 bilioni
Nigeria - Sukari, Saruji na Unga
Aliko Dangote ndiye mtu tajiri zaidi mweusi duniani na mtu tajiri zaidi Afrika.
Alianzisha kampuni ya Dangote Cement nab ado ndiye mwenyekiti wa kampuni hiyo. Dangote Cement inaongoza kwa kutengeneza saruji Afrika.
Dangote anamiliki kampuni pia za sukari, chumvi na za kusaga unga.
Kampuni yake ya Dangote Group inajenga kiwanda cha kusafisha mafuta karibu na Lagos, Nigeria ambacho kitakapomaliza kujengwa mwaka 2019 kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi cha aina yake duniani. Kiwanda hicho kitagharimu $9bn.
Presentational grey line
2. Mike Adenuga, $5.3 bilioni
Nigeria- Mafuta
Utajiri wake umetokana na mafuta, sekta ya mawasiliano, nyumba na ardhi na sekta ya benki. Hufahamika sana na wenzake kama Guru.
Globacom kampuni yake ya mawasiliano ndiyo ya pili kwa ukubwa Nigeria baada ya MTN ambapo ina zaidi ya wateja 30 milioni.
Kampuni yake ya mafuta ya Conoil Producing ni moja ya kampuni za wenyeji wa Afrika zinazoongoza katika kupeleleza na kuzalisha mafuta Nigeria. Adenuga ndiye pia anayeongoza kwa umiliki wa mali Nigeria na Ghana, kama mtu binafsi. Ana hisa katika kampuni ya ujenzi ya Julius Berger.
Presentational grey line
3. Robert Smith, $4.4 bilioni
Marekani- Uwekezaji na Usimamizi wa Mali
Ni mfanyakazi wa zamani wa Goldman Sachs na alianzisha kampuni ya uwekezaji ya Vista Equity Partners yenye makao yake Austin, Texas mwaka 2000. Kufikia sasa, anasimamia uwekezaji wa zaidi ya $30 bilioni na ni miongoni mwa wanaosimamia hazina zilizofanikiwa zaidi duniani. Mwaka 2016, aliahidi kutoka $50 milioni kwa chuo alichosomea, Chuo Kikuu cha Cornell.
Oprah Winfry akitabasamu baada ya hotuba yake katika tuzo za Golden GlobeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionOprah Winfry akitabasamu baada ya hotuba yake katika tuzo za Golden Globe
Presentational grey line
4. Oprah Winfrey, $2.7 bilioni
MarekaniRuninga
Alikuwa Mwafrika Mmarekani tajiri zaidi kwa muda lakini kwa sasa Oprah hana taji hilo tena. Alijipatia utajiri mwingi akifanyakazi kwenye runinga. Alianza kuchangia kama mchangiaji maalum kipindi 60 Minutes mwishoni majuzi. Runinga yake ya kulipiwa ya OWN (Oprah Winfrey Network) kwa sasa inatengeneza faina. Anamiliki hisa 10% katika kampuni ya Weight Watchers na hufanyishwa kazi kama balozi wa nembo mbalimbali.
Isabel dos Santos ni binti wa rais wa Angola
Image captionIsabel dos Santos ni binti wa aliyekuwa rais wa Angola
5. Isabel Dos Santos, $2.6 bilioni
Angola - Uwekezaji na Mafuta
Ndiye mwanamke tajiri zaidi Afrika na mambo yalikuwa yakimwendea vyema wka muda mrefu. Babake alikuwa Rais wa nchi hadi alipostaafu mwaka jana naye alikuwa mwenyekiti wa shirika la mafuta la taifa Sonangol. Novemba mwaka jana, Rais mpya João Lourenço alimpokonya uenyekiti huo na anachunguzwa na maafisa wa serikali kuhusiana na ubadhilifu wa fedha. Amekanusha tuhuma hizo.
Isabel dos Santos anamiliki hisa katika Unitel, kampuni ya simu iliyo kubwa zaidi Angola na ana pia hisa katika Banco BIC. Ana hisa katika Galp Energia na Banco BPI. Ndiye mwenyehisa mkuu katika kampuni ya runinga na mawasiliano ya simu Ureno Nos SGPS.
Presentational grey line
6. Patrice Motsepe, $2.5 bilioni
Afrika Kusini - Madini
Patrice Motsepe ni mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa African Rainbow Minerals kampuni ambayo imewekeza sana katika uchimbani na uuzaji wa madini Afrika Kusini. Ndiye mwanzilishi wa kampuni ya uwekezaji ya African Rainbow Capital ambayo huwekeza katika kampuni za kifedha. Ndiye mmiliki wa klabu ya Mamelodi Sundowns.
Presentational grey line
7. Folorunsho Alakija, $1.7 bilioni
Nigeria - Mafuta
Ndiye mwanamke tajiri zaidi Nigeria na naibu mwenyektii wa kampuni ya upelelezi wa mafuta ya Famfa Oil.
Alakija alianza akiwa katinu katika benki moja Nigeria miaka ya 1970 kisha akaacha kazi na kwenda kusomea mitindo England. Aliporejea, alianzisha kampuni ya mitindo ya kifahari ya ambayo miongoni mwa wengine wateja wake walikuwa Maryam Babangida, mke wa kiongozi wa zamani wa kijeshi Ibrahim Babangida.
Presentational grey line
8. Michael Jordan, $1.65 bilioni
Marekani - Mpira wa kikapu
Ndiye mchezaji aliyefanikiwa zaidi katika mpira wa kikapu na mwenyehsia mkuu katika Charlotte Bobcats.
Ana mikataba ya pesa nyingi na kampuni kama vile Gatorade, Hanes na Upper Deck. Pesa zake nyingi kwa sasa hujipatia kutoka kwa Brand Jordan, ushirikiano wake na Nike katika mavazi ya kimichezo ambao una thamani ya $1 bilioni.
Presentational grey line
9. Strive Masiyiwa, $1.39 bilioni
Zimbabwe-, Mawasiliano
Ndiye bilionea wa kwanza kutoka Zimabbwe na amewekeza zaidi katika mawasiliano.
Masiyiwa, 57, ndiye mwanzilishi wa kampuni ya simu ya Econet Group.
Amewekeza pia katika sekta ya huduma za kifedha, bima, uchumi, nishati mbadala, elimu, kuweka chupa soda za Coca Cola, hoteli na utalii na huduma za malipo ya bidhaa na huduma.
Econet pia humiliki Kwesé TV ambayo imekuwa ikishindana na DSTV Afrika.
Presentational grey line
Mo IbrahimHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionMo Ibrahim
10. Mohammed Ibrahim, $1.18 bilioni
Mwingereza - Mawasiliano ya simu, Uwekezaji
Mo Ibrahim, 71, alipata pesa zake za kwanza nyingi kuptiia kuanzisha kwa kampuni ya mawasiliano ya simu ya Celtel ambaye baadaye aliiuza kwa MTC ya Kuwait kwa $3.4 bilioni mwaka 2005.
Alijizolea $1.4 bilioni. Kwa sasa amewekeza kupitia Satya Capital, kampuni ya uwekezaji yenye makao yake Uingereza lakini huangazia uwekezaji Afrika.
Duniani kwa jumla, anayeongoza orodha ya matajiri wa kupindukia ni mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos.
Utajiri wa Bezos umepanda na kufikia $112bn kutoka takriban $39.2bn mwaka jana.
Kuimarika kwa utajiri wa Bw Bezos ndiko kwa juu zaidi katika historia.
Amemuondoa mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kutoka uongozini kwenye orodha hiyo.
Utajiri wa Gates unakadiriwa kuwa $90bn mwaka huu kutoka $86bn, na ndiye anayeshikilia nafasi ya pili.
Bw Gates ameongoza orodha hiyo kwa miaka 18 kati ya miaka 24 iliyopita.
Matajiri

Post a Comment

0 Comments