Jimbo la California limewaamuru wakazi wake "kukaa nyumbani" huku likijaribu kudhibiti maambukizi ya coronavirus katika jimbo hilo maarufu zaidi nchini Marekani.
Govana Gavin Newsom aliwaambia wakazi wa California kuwa watatakiwa kuondoka majumbani mwao tu wakati ni muhimu wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.
Awali alikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 40 katika jimbo lake wanaweza kupata maambukizi ya virusi vya Covid-19 katika miezi miwili ijayo.
Virusi vya corona tayari vimewaua watu 205 nchini Marekani huku watu 14,000 wakipata maambukizi.
Kwa ujumla wagonjwa karibu 250,000 kote duniani wamepatikana na virusi hivyo vinavyosabisha ugonjwa kupumua na takriban 9,900 wamekufa.
Amri ya California inamaanisha nini
Gavana Newsom alisema siku ya Alhamis jioni: "Wakati huu tunahitaji kuchukua maamuzi magumu.Tunahitaji kutambua hali halisi."
Amri yake itawaruhusu wakazi kuongoka majumbani mwao kununua mahitaji ya nyumbani au dawa, au pale wanapotembeza mbwa au wanapofanya mazoezi ya mwili, lakini itawataka kuacha mikusanyika ya watu.
Itawalazimisha biashara ambazo zinaonekana si za lazima kufungwa, huku ikiwaruusu wengine wanaofanya biashara za vyakula na mahitaji na bidhaa nyingine muhimu za nyumbani, maduka ya dawa, benki na vituo vya mafuta ya petroli kuendelea kufunguliwa.
Takriban nusu ya wakazi wa jimbo hilo wamekwishaanza kutekeleza hatua hizo kali, mkiwemo Jiji la San Francisco.
- Kila kitu unachohitaji kufahamu kuhusu coronavirus
- Kwanini kunawa mikono ni vigumu katika baadhi ya nchi
- Majibu ya maswali 10 yanayoulizwa sana kuhusu coronavirus
- Visa vya Coronavirus vyaongezeka Tanzania, huku WHO ikionya Afrika
Gavana Newsom ambake anatoka chama cha Democratic vamesema kuwa sehemu za jimbo hilo zimeshuhudia kuongezeka kwa viwango vya maambuzi ya coronavirus mara dufu kwa kila baada ya siku nne.
Alielezea ubashiir wake katika barua kwa rais Donald Trump siku ya Jumatano, akitoa wito wa msaada wa haraka kutoka kwa Serikali ya kuu.
"Tunatazamia takriban asilimia 56 ya watu- milioni 25.5 wataathiriwa na virusi vya cporona katika kipindi cha wiki nane zijazo ," Gavana Newsom aliandika.
Hadi sasa California imerekodi visa vilivyo chini kidogo ya 1,000 vya virusi vya corona na vifo 19, kwa mujibu wa gazeti la Los Angeles Times.
Maeneo mengine yenye ''idadi kubwa'' ya coronavirus ni yapi?
Kando na Jiji la New York na Washington, California ni miongoni mwa majimbo yaliyozongwa na janga la coronavirus.
Alhamisi pekee, rekodi ya maambukizi ya Covid-19 katika Jiji la New York ilionyesha kuongezeka mara dufu na kufikia hadi watu 3,954 - ikiwa ni kubwa kuliko watu idadi ya wagonjwa wa coronavirus katika nchi nzima ya Uingereza.
Meya Bill de Blasio aliiambia CNN kuwa jimbo hilo maarufu nchini Marekani litakosa vifaa vya kimatibabu katika kipindi cha wiki tatu ikiwa ''mlipuko'' wa maambukizi utaendeela kwa kiwango cha aina hiyo.
Aliitaka serikali ya shirikisho kuisaidi New York kupata vifaa vya kusaidia kupumua 15,000, barakoa za upasuaji milioni 50 , na magauni ya 45 million, na vifaa vya madaktari vya kujikinga.
Meya alisema kuwa virusi vimewaua watu 26 katika jiji hilo..
Wakati huo huo wizara ya mambo ya nje ya Marekani Alhamisi iliwataka Wamarekani kuacha safari za nje ya nchi.
0 Comments