Coronavirus: Je, virusi vya corona vimetengenisha watu na imani zao?




msikiti wa MeccaHaki miliki ya pichaABDEL GHANI BASHIR
Image captionIdadi ya watu waliohudhuria hija Mecca wamepungua kwa kiasi kikubwa

Kutokana na kuenea kwa kasi kwa virusi vya corona, watu katika maeneo mbalimbali duniani wameanza kubadili mwenendo wao wa kufanya mambo.
Baadhi ya watu wamehairisha mipango yao ya kusafiri na kujizuia kufika katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu.
Wengine wameacha kusalimiana kwa kushikana mikono na kukumbatiana , huku wengine wakibuni namna mpya ya kusalimiana kwa kugonga miguu.
Taratibu za kwenye Makanisa, misikiti na mahekalu pia zimebadilika,zikiwa ni jitihada za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.
Je, ni rahisi kiasi gani kubaki katika hali hiyo na kuwafanya watu wabadili namna yao ya kuabudu?
Waislamu


Baadhi ya waumini wakiwa wamevaa mask wakisali ibada ya ijumaa nje ya msikiti wa MeccaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWaumini wakisali mbele ya msikiti wa Mecca baada ya msikiti huo kufungwa kwa muda

Msikiti mkubwa ulioko Mecca, mara zote huwa umejaa maelfu ya waumini ambao ufika hapo kwa ajili ya hija.
Lakini sasa idadi ya mahujaji ambao wamefika katika eneo hilo takatifu imeshuka kupita kiasi.
Hatahivyo msikiti huo mkubwa umefunguliwa baada ya kufungwa kwa muda ingawa sasa kuna sheria mpya za kuabudu katika eneo hilo kama vile, katazo la watu kuzungukia 'kaaba' ambayo iko katika ya msikiti na kuzuia watu kupashika.
Katazo hilo limetolewa kwa mahujaji wote wageni na wenyeji wa Mecca na Medina.
Waumini wengi kutoka maeneo mbalimbali duniani mara nyingi huwa wanatembelea katika eneo hilo la hija hata kama sio wakati wa hija.
Waislamu wapatao muilioni nane ufanza ziara za kwenda Mecca kuiji kwa mwaka.


Maujaji wakiwa wamezunguka Kaaba (Tawaf al-Wadaa)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEneo takatifu la Saudi mara nyingi huwa limefurika maujaji wengi wa kiislamu

Hadiza Tanimu Danu ana biashara ya wakala wa usafiri nchini Nigeria ambayo imejikita kaika safari za kwenda Mecca, na kusema kuwa katazo la wageni limechanganya watu.
"Watu wana huzuni" aliniambia. "Unajua si kila mtu anataka kwenda huko kwa minajili ya kwenda kuabudu, bali wengine wana nia nyingine."
Si Umrah peke yake ndio inaathirika.
"Baadhi wana hofu kuwa hali hii itaendelea mpaka wakati wa Radhani, na kama hali hii itaendelea hata wakati wa Hija, je nini kitatokea?" alisema.
Mamlaka ya Saudia inasema kuwa hatua waliyochukua ni ya muda mfupi na haiashirii kuwa wanapanga kufanya hivyo hata wakati wa Hija.
Baadhi ya taratibu za kusali ambazo zinaweza kusababisha maambukizi bado zinaendelea.





Mambo matano muhimu kuhusu virusi vya corona

Kulikuwa na tahadhari duniani kote baada ya video ya raia wa Iran ambayo ilisambaa katika mtandao wa kijamii.
Ikimuonyesha muumini mmoja akisema kuwa siogopi virusi vya corona kabla ya kulamba na kubusu geti. Baadhi ya watu huwa wanaamini kuwa eneo takatifu ni salama na kunaweza kukuponya na magonjwa.
Watu wawili wamejikuta gerezani kutokana na imani zao lakini wairani wanasema kuwa maeneo ya Iran yanapaswa kuwa yamefungwa.
Kwa waislamu wengi, licha ya kwamba mabadiliko ni kidogo lakini wanajaribu kuzingatia mabadiliko hayo.
Kwa mfano , Afrika kusini wanakabiliana na kesi moja ya virusi vya corona, viongozi wa dini wanatumia fursa ya kuelimisha watu kujikinga na corona wakati wa ibada
Mwandishi wa BBC Afrika, Mohammed Allie anasema kuwa waumini katika misikiti wameshauriwa kutoshikana mikono au kukumbatiana baada ya ibada.
"Itaenda kuchukua muda kwa watu kuzoea utaratibu huo," alisema.
"Watu bado wanapeana mikono baada ya kutoka msikitini, na sio kwa sababu wanadharau ujumbe waliopewa bali ni utamaduni ambao wameuzoea sana."
Amesema baadhi ya watu wameanza kugusana miguu badala ya mikono.
"Taratibu watu wameanza kuzoea," alisema na kuongeza kuwa wauimini Singapore wameshauriwa kuja na mikeka yao wenyewe kwa ajili ya kusalia siku ya Ijumaa.

Ukristo



Kanisani kuna chupa ya 'sanitizer' mlangoni mwa kanisa huko Bangkok.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUtaratibu wa kanisani umebadilika duniani kote kwa sababu ya virusi vya corona

Mamia ya watu ambao wanahudhuria misa huko Georgetown, kanisa la kihistoria lililopo Marekani katika mji mkuu wa Washington D.C. ambalo limewekwa karantini baada ya muumini mmoja wa kanisa hilo kuthibitishwa kuwa mgonjwa wa virusi vya corona.
Padre Timothy Cole alikutwa ana virusi vya corona siku ya jumamosi na a kawekwa karantine yeye pamoja na familia yake.
Imeripotiwa kuwa watu wapatao 550 walikuepo katika ibada ya Machi, 1 na kupokea komuniyo.
Huko Italia, Papa Francis ameamua kusaisha misa siku za jumapili akiwa anaonekana kwenye video kutokea dirishani katika makutano ya St Peter na kuachana na misa alizokuwa anazifanya mubashara ili tu kupunguza idadi ya mkusanyiko wa watu mjini Vatican.


Pope Francis live streaming prayers on giant screens in St Peter's squareHaki miliki ya pichaALBERTO PIZZOLI
Image captionPapa Francis akiendesha misa

Hatua hii imekuja baada ya watu kaskazini mwa Italia kuwekwa katika karantini.
Makanisa ya katoliki kuanzia Ghana, Tanzania mpaka Marekani na Ulaya wamebadili utaratibu wa ibada zao ikiwa ni jitihada za kuzuia maambukizi.
Mapadre sasa wanawapa waumini ekaristi takatifu katika mikono badala ya ulimi, wameacha kutoa divai na kuwa na dawa ya kuzuia maambukizi mlangoni sehemu ya kuchovya maji ya baraka(senitizer).
Badala ya kupeana mikono kama ishara ya amani, waamini wanaambiwa kumuombea jirani yake.
Lakini pamoja na kwamba wanaelewa kwa nini hatua hizo zinachukuliwa lakini bado wanaonekana kutoelewa bado.
Alexander Seale ni muandishi wa Ufaransa anayeishi London anasema;
"Hakuna furaha kama ilivyokuwa awali," aliniambia, " kwenda kanisani bila kuonyesha ishara ya amani na bila kulishwa ekaristi mdomoni na padre ni sawa na kuondoa sehemu muhimu katika ibada takatifu."
"Kwangu binafsi, mimi kula ekaristi takatifu ni kitu cha thamani sana, Ni sawa na kupokea mwili wa Yesu."
"Inasikitisha sana kuona hatua hizo zimechukuliwa ."
Na hii ikiwa ni matokeo ya kusambaa kwa virusi vya corona.
Huko Korea kusini, zaidi ya nusu ya visa vyote katika nchi hiyo vimehusishwa na makundi ya kikristo katika makanisa.
Ilidhaniwa kuwa kukaa karibu sana na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya corona kunaweza kumfanya mtu apate maambukizi kwa haraka na vilevile mtu anayesafiri katika maeneo mbalimbali duniani kunaweza kumfanya aambukize wengine.
Viongozi wa kanisaniwamekuwa wakishutumiwa kuficha majina ya watu waliopata maambukizi hivyo kufanya mamlaka kushindwa kupata waathirika kabla maambukizi hayajasambaa.
Kesi hii ni ya aina yake na makanisa duniani kote wanapaswa kuchukua hatua thabiti ya namna gani wanaweza kufanya kazi na serikali ili kuzuia maambukizi.

Wabaniani



Holi revellers wearing face masks to protect against COVID-19Haki miliki ya pichaSANJAY KANOJIA
Image captionWamevaa mask kwakati wa ibada kujikinga na COVID-19

Kwa wabaniani, kipindi hiki huwa wanasheherekea tamasha la rang.
Huwa wanaadhimisha mema , upendona maisha mapya.
Watu hujipaka rangi katika sura zao pia ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo.
Waziri mkuu wa India bwana Narendra Modi alisema kuwa sherehe hizo hazitafanyika katika sehemu ya umma, na kushauri watu kujizuia kuwa katika msongamano wa watu wengi.
Lakini watu wengi hawakuhudhuria tamasha hilo mwishoni mwa wiki iliyopita na baadhi walioenda walikuwa wamevaa masks.
Hali hii ni ya hatari ambayo walikuwa hawajajiandaa kuchukua.
Nicky Singh anaishi Amritsar, katika jimbo la Punjab, India. Anasema kuwa alibaki nyumbani na kutuma salamu za sherehe hizo kwa simu.
Aliniambia kuwa sherehe hizo zilikosa msisimko waliouzoea wa Holi".
"Nina furahi kuwa nilichagua afya yangu badala ya sherehe" alisema.

Wayahudi



Indian Jewish man with his child touching the mezuzah at synagogueHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWayahudi wengi huwa wanabusu hekalu kwakati wanaingia kusali

Lakini unawaambiaje watu waache kukumbatiana wakati wa majonzi kwenye misiba? alisema hivyo Rabbi Jackie Tabick, kutoka magharibi mwa London.
"Ni ngumu sana," aliniambia.
"Nadhani kila mtu huwa anataka kuonyesha hisia zake kwa mfiwa, na njia nzuri ya kuonyesha upendo siku hizi ambayo kila mtu anaielewa ni kukumbatia na kuongea inawezekana si jambo ambalo mfiwa angependa wakati wa majonzi."
Yeye anapanga kutoa mafunzo mtandaoni, kuona namna gani tunahakikisha umuhimu wa kuungana mono na kuungana na Mungu.

Post a Comment

0 Comments