Ni kama dunia inataka kuzima. Maeneo ambayo kulikuwa na hekaheka nyingi za maisha ya kila siku.
Sasa hali imekuwa tofauti, miji imekuwa kimya kama miji ya mizimu ambapo kwengine hakuna watu barabarani na shughuli zikiwa zimesitishwa huku kukiwa na makatazo mengi.
Makatazo kuanzia kwenye shule, usafiri na mikusanyiko ya watu kuzuiwa hata sehemu za ibada au burudani.
Swali ni lini ugonjwa huu wa corona utaisha?
Lakini haijajulikana pia ni lini hali hii ya hofu dhidi ya corona itaondoka katika maisha yetu?
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson anaamini kuwa mlipuko huu unaweza kupata chanjo ndani ya wiki 12 zijazo.
Huku idadi ya kesi za corona zitaanza kupungua katika miezi mitatu ijayo, hivyo bado tutakuwa mbali kufikia hatima ya janga hili.
Mlipuko wa ugonjwa huu unaweza kuchukua muda mrefu kuondoka hata mwaka mzima unaweza kupita.
Iko wazi kuwa , maeneo mengi ya umma yamefungwa au hayafanyi kazi kwa muda usiofahamika.
Shughuli za kijamii na kiuchumi zimedorora na zatarajia kuathiri dunia kwa kiwango kikubwa.
Maswali ni mengi bila majibu...
Ni nchi gani inahitaji kuwa na mikakati ya kuondoka katika janga hili?
Ni namna gani watu wanaweza kurudi katika hali ya kawaida na mataifa kuachana na makatazo ya kila kukicha.
Lakini je, virusi vya corona havitaondoka?
Kama wataacha kuzingatia makatazo yaliyowekwa basi visa vya ugonjwa huu vitaongezeka.
"Tuna tatizo kubwa na kuondoka katika tatizo hili pia ni changamoto kubwa," alisema bwana Mark Woolhouse, Profesa wa magonjwa ya maambukizi katika chuo kikuu cha Edinburgh.
"Tatizo halipo Uingereza peke yake, hakuna taifa ambalo lina mikakati ya kujinasua kutoka katika janga hili."
Ni changamoto kubwa kwa wanasayansi na janga kubwa kwa jamii kwa ujumla
Kuna namna tatu za kukabiliana na tatizo hili.
- Chanjo
- Idadi ya kutosha kuwa na kinga ya kuepuka maambukizi
- au kubadili mifumo ya maisha yetu
Njia hizo zinaweza kuzuia maambukizi kusambaa kwa wingi.
Chanjo - kupatikana ndani ya miezi 12-18
Chanjo inaweza kumpa mtu kinga, ya kujizuia kupata gonjwa kama akikumbana na maambukizi .
Watu wengi wakipata chanjo kama kinga , kwa watu wapatao asilimia 60% hivi , basi virusi haviwezi kusababisha milipuko kutokea.
Mgonjwa wa kwanza kupewa chanjo kama jaribio nchini Marekani wiki hii baada ya watafiti kusema kuwa waliruhusiwa kuacha kutumia mlolongo ambao huwa wanatumia kila wakati kwa kutumia vipimo vya wanyama.
Utafiti wa chanjo unafanyiwa kwa haraka lakini hakuna uhakika lini wataweza kufanikiwa kupata kinga hiyo duniani kote kwa ujumla.
Kama chanjo itawezekana kupatikana kama ilivyopangwa kwa miezi 12-18, basi kila kitu kitaenda sawa.
Bado hakuna uhakika wa lini watu wataendela na shughuli zao na amani ikarejea kwa watu.
"Kusubiriwa kwa chanjo kusiwe kuwa jambo ambalo ni moja ya mkakati," Prof Woolhouse aliiambia BBC.
Kinga ya asili - kwa takribani miaka miwili ijayo
Tunazungumzia matumaini kidogo ya kuweza kukabiliana na janga hili.
Swali kubwa ni kinga ikiwepo itadumu kwa muda gani.
Virusi vingine vya corona huwa vina dalili ya mafua ambavyo huwafanya watu kupata mara kwa mara.
Njia mbadala - hakuna uhakika wa mwisho wake
"Njia nyingine ambayo watu wanapaswa kufuata ni kuweka mabadiliko ya moja kwa moja ya kupunguza kiwango cha maambukizi.
Hii ni pamoja kuendelea kuchukua tahadhari ambazo tumepewa tayari kama vile kuzingatia usafi na kujikinga na watu ambao wameambukizwa.
Kama dawa ya ugonjwa huu wa corona ikifanikiwa kupatikana basi itaweza kusaidia mipango mingine ya kukabiliana na janga hili.
Kama dalili zikiweza kutambuliwa mapema na kuzuiliwa kwa maambukizi kwa wengine.
Matumaini bado yapo kwa chanjo na wanasayansi duniani kote wanategemewa kuja na suluhu ya janga hili.
0 Comments