Kansela wa Ujerumani, Bi. Angela Merkel ameonya kuwa hadi 70% ya watu nchini humo - karibu watu milioni 58 - huenda wakaambukizwa virusi vya corona .
Bi. Merkel ametoa tamko hilo katika taarifa kwa wanahabari siku ya Jumatano akiwa na waziri wa afya, Jens Spahn.
Amesema kwa sababu hakuna tiba iliyopatikana kufikia sasa,mikakati zaidi inatakiwa kuelekezwa katika udhibiti wa kusambaaa kwa virusi hivyo "Cha msingi ni juhudi za kukabiliana nao haraka iwezekanavyo,"alifafanua.
- Waziri wa afya Uingereza akutwa na maambukizi ya virusi vya corona
- Unawezaje kujitenga binafsi kuzuia kuambukiza virusi vya Corona?
Tamko lake linajiri wakati ambapo Italia imeingia siku ya pili ya kuweka karantini ya kitaifa.
Mgonjwa wa tatu afariki Ujerumani
Ujerumani ilithibitisha kisa cha tatu cha maambukizi ya virusi vya corona pamoja na kifo kinachohusiana na kirusi hicho siku ya Jumatano katika wilaya ya Heinsberg magharibi iliyopo katika jimbo la Rhine-Westphalia .
Kifo cha kwanza kilikuwa cha mwanamke wa miaka 89 ambaye alifariki katika mji wa Essen, na cha pili kilikuwa cha mwanaume wa miaka 78 aliyekuwa na changamoto za kiafya ambaye alifariki katika mji wa Heinsberg.
Ujerumani imeripoti visa 1,296 vya maambukizi ya virusi vya corona, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa siku ya Jumanne naTaasisi ya Robert Koch (RKI) ambayo inasimamia masuala ya kudhibiti.
Rais wa RKI, Lothar Wieler amesema taasisi hiyo haiamini kuna visa vingi vya maambukizi ambavyo havijagunduliwa nchini humo.
Katika taarifa yao ya kwanza kwa vyombo vya habari kuhusu mlipuko wa virusi hivyo Bi Wieler - na Chancellor Merkel wameonya hatua ya kufunga mpaka pekee hakutasaidia kudhibiti maaambukizi ya virusi hivyo, na kupuuzilia mbali madai kwamba wameiga hatua ya Austria ya kuwapiga marufuku wageni kutoka Italia.
"Huu ni mtihani unaopima umoja wetu, na ipo haja ya kila mmoja wetu kutilia maanani maslahi na kuona umuhimu wa kujali afya ya kila mmoja wetu. Na kuwa na matumaini kwamba tutapita mtihani," alisema.
Nini kinachofanyika kwingine duniani?
Gavana wa New York ametangaza kuwa wanajeshi watapelekwa katika mji wa kaskazini wa New Rochelle, katika juhudi za kudhibiti mlipuko wa virusi huku visa vya maambikizi nchini Marekani vikipita 1,000 siku ya Jumatano.
Athari kubwa imeonekana nchini China. Lakini siku ya Jumapili iliripoti idadi ya chini zaidi ya maambukizI mapya katika siku moja tangu Januari - ishara kwamba kuenea kwa virusi kunapungua.
Iran, moja ya maeneo yenye maambukizi mabaya zaidi nje ya China, sasa imethibitisha maambukizi 6,566 na vifo 194.
Hatahivyo, takwimu halisi zinakisiwa kuwa za juu zaidi. Ripoti moja Jumapili, ikinukuu mjumbe wa serikali, ikisema kulikuwa na vifo 200 katika mkoa wa kaskazini wa Gilan pekee - lakini takwimu hizo baadaye ziliondolewa.
Huko Ufaransa, virusi vinaenea miongoni mwa wabunge. Wabunge wawili walikutwa na maambukizi, maafisa walieleza siku ya Jumapili.
Kwa jumla manaibu wanne wameambukizwa. Pia Jumapili Ufaransa iliripoti visa 1,126, ongezeko la 19% kwa siku na idadi kubwa ya maambukizi barani Ulaya baada ya Italia.
Serikali ya Ufaransa imepiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 1,000.
Nchini Marekani, zaidi ya watu 470 wamekutwa na maambukizi ya Covid-19 na mpaka sasa waliopoteza maisha ni watu 21.
Miongoni mwa nchi zilizoripoti ongezeko la maambukizi ni Ujerumani 939, Uhispani 589, Uingereza 273 na Uholanzo 265.
Albania, Bulgaria, Colombia, Costa Rica, visiwa vya Maldives, Malta, na Paraguay zimeripoti visa vya kwanza vya maambukizi ya virusi hivyo.
0 Comments