VIDEO | Mmzy - Dominate


 
Kutoka Nchini Nigeria Kutana Na Msanii Mwenye Uwezo Wa Kitofauti Katika Uimbaji Wake Ambaye Licha Ya Kuweza Kutumia Lugha Za Naijeria Pia Anatumia Kiingereza Pamoja Na Kifaransa Katika Nyimbo Zake Jambo Ambalo Linavutia Mashabiki Kutoka Mataifa Mbalimbali Katika Uimbaji Wake. Anaitwa Mmzy Ambaye Amefanikiwa Kufanya Kazi Nyingi Nzuri Ikiwemo Miracle Lover,Wildin,Animal Na Sasa Amerejea Tena Na Wimbo Mwingine Alioupa Jina La “Dominate “ Ni Wimbo Ambao Kwa Asilimia Kubwa Umeelez Namna Alivyoweza Kutoka Kwao Na Kwenda Jijini Lagos Kutafuta Riziki Ambayo Amefanikiwa Kuipata Kwa Kiasi Fulani. Wimbo Huu Umetayarishwa Na Mtayarishaji Wa Nyimbo Kutoka Naijeria Ambaye Amefanya Kazi Na Wasanii Wakubwa Kama Vile,Yemi Alade,Mr Flavour ,P Square,Patoranking Na Wengine Wengi Si Mwingine Bali Ni Masterkraft. Karibu Kutazama Wimbo Huu Na Unaweza Kuupata Katika Vyanzo Mbali Mbali Vya Muziki Kupakua Na Kusikiliza,Pia Unaweza Kumpata Mmzy Kupitia Mtandao Wa Instagram @Realmmzyofficial.             

Post a Comment

0 Comments