Famlia na marafiki wanasubiri taarifa mjini Nairobi kuhusu hatma ya wapendwa wao waliokua wamesafiri kwa ndege ya Ethiopia iliyopata ajali leo jumapili asubuhi.
Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili mjini Naorobi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo kanyatta saa nne unusu kwa saa za Afrika Mashariki.
Taarifa ya Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines imesema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege iliyopata ajali wote wamekufa, kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat Begashaw.
Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.
i.
Taarifa ya Shirika la ndege la Ethiopia- Ethiopian Airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adi Ababa.
Takriban wasafiri 149 na wahudumu wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hakuna hata mmoja aliyeweza kunusurika na wote wamekufa, aliliambia shirika la habari la kitaifa la Ethiopia msemaji wa Ethiopian Airlines.
Waathiriwa ni akina nani?
Mkurugenzi mtendaji wa Ethiopian Airlines CEO Tewolde Gebremariam ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba miongoni mwa waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na :
Wakenya32 Kenyans, raia wa Canada 18 raia tisa wa Ethiopia , wataliano wanane , Wachina wanane, wamarekani wanane , waingereza saba , Wafaransa saba , Wamisri sita, Wajerumani watano , Wahindi wanne na wanne kutoka Slovakia.
Waastralia watatu, Waswis watatu, Warusi watatu , three Russians, Wakomoro wawili, Wahispania wawili, Wapoland wawili, Waisraeli wawili.
Kulikuwa pia abiria mmoja mmoja kutoka nchi za ubelgiji, Indonesia, Somalia, Norway, Serbia, togo, Msumbiji, rwandsa, Sudan, Uganda na Yemen.
Afisa wa itifaki wa Somalia ameripotiwa kuwa mmoja wa watu waliokufa kwenye ajali hiyo , kulingana na kituo cha kibinafsi cha Radio Dalsan, kinachomilikiwa na redio ya Somalia.
'Wachina wanane walikuwemo katika ndege hiyo', kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo.
Raia wanane wa uchina walimetambuliwa kuwa walikuwemo ndani ya ndege ya Ethiopian Airlines, imesema taarifa ya vyombo vya habari vya Uchina.
Awali Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines inasema imeanzisha kituo cha kupata taarifa kuhusu familia na marafiki za watu waliliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Ofisi ya waziri Mkuu wa Ethiopia Abey Ahmed imetoa taarifa ikitoa rambi rambi kwa familia za walio wapoteza wapendwa wao katika jali hiyo.
''Kasi haikuwa thabiti''
Kituo cha ufuatiliaji wa safari za ndege kwa kwa saa 24 imekuwa kikitoa taarifa kwneye ukurasa wake wa twitter juu ya ajali ya ndge ya Ethiopian Airlines.
Kimesema kuwa kilibaini kuwa " kasi ya ndge hiyo ya wima haikuwa thabiti baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege ".
Ndege hiyo ambayo ilitarajiwa Nairobi iliondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa saa 8:38 asubuhi kwa saa za Ethipia lakini ikapoteza mawasiliano majira ya saa 8:44 asubuhi kwa saa za Ehiopia.
Kampuni ya Kenya Airways imetoa rambi rambi zake kufuatia ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines. Mkurugenzi mkuu wa Kenya Airways Sebastian Mikosz ametuma salam zake za rambi rambi kupitia ukurasa wa Twitter kwa familia na wale waliowapoteza wapendwa wao kwenye ajali hiyo.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia ametoa rambi rambi zake kupitia ukurasa wa twitter kwa waathiriwa wa ajali ya ndege ya Ethiopia akiwapa pole familia pamoja na wote walioguswa na ajali hiyo.
Ndege hiyo ya Boeing 737 Max-8 ilikua ni mpya
Boeing, kampuni ambayo iliitengeneza ndege iliyoanguka , imesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba 'inafuatilia kwa karibu hali' ya mambo.
Ndege ya 737 Max-8 ni mpya angani , ikiwa ilizinduliwa kwa mara ya kwanza 2016. Iliongezwa kwenye safari za ndege za Ethiopian Airlines Julai mwaka jana.
Boeing imesema ''imesikitishwa sana'' na ajali na imejitolea kutuma kikosi cha wahandisi wake kutoa usaidizi wa kiufundi.
Ndege nyingine iliyotengenezwa kwa muundo wake ilianguka miezi mitano iliyopita, wakati safari ya ndege ya Lion Air ilipoangukia baharini karibu na Indonesia ikiwa imewabeba wasafiri 190.
Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi kuhusu tukio hili . Fuatilia taarifa hii kupata maelezo zaidi.
0 Comments