Ellie na Nele: Wabadili jinsia kutoka ya kike hadi kiume na kurejesha ya kike tena

Presentational white space
Utafiti unaonesha kwamba watu wengi ambao wanabadilisha jinsia huwa hawafikiria mara mbili. Lakini baada ya wanaume wawili waliobadili jinsia zao kukutana na kupenda, safari yao ilichukua mkondo mpya ambao haukutarajiwa.
"Kila wakati nilikuwa nikihisi tuna historia ya kipekee. Tuna miili ya kipekee ushirikiano wetu ni wa kipekee kwa kuzingatia uzoefu wa mwili wetu ulivyokuwa."
Ellie ana umri wa miaka 21 na mpenzi wake mjerumani, Nele, 24. Wote walianza kutumia homoni za testosteroni na kuwa na muonekano wa kiume zaidi na wakaamua kufanyiwa upasuaji wa kuondoa matiti.
Kwa sasa wawili hao wamebadilisha tena jinsia zao na wameanza tena kuishi kama wanawake jinsia ambazo ndizo walizopewa baada ya kuzaliwa.
"Ninafurahi kwasababu sikuendolewa tumbo langu la uzazi," Nele anasema. "Hii inamaanisha kwamba ninaweza kuacha kutumia homoni hizi, na mwili wangu utaanza taratibu kurejea kuwa kama wa mwanamke."
Mwaka jana, wote waliamua kuacha kutumia homoni za testosteroni na wakaanza kutumia viwakilishi vya mwanamke tena. Taratibu homoni zao za asili za estrojeni zimeanza kurejesha miili yao kuwa ya kike.
"Nina hamu sana ya kutaka kuona mabadiliko kamili," amesema Ellie.
Nyuso zao zimeanza kuwa na laini na miili yao imeanza kuwa umbo la kike. Lakini baada ya miaka kadhaa ya kutumia homoni za testosteroni kumekuwa na athari moja kubwa ambayohaiwezi kurekebishika.
"Sauti yangu haiwezi kurejea kuwa laini jinsi ilivyokuwa," anasema Nele."Nilikuwa ninapenda kuimba lakini kwa sasa ziwezi kuimba tena - sauti yangu imekuwa nzito na isiyopendeza, tofauti kabisa a ilivyokuwa. Ninapompigia mtu simu, ninayempigia hunitambua kama mwanaume."
Ellie hakumbuki wakati akiwa mtoto alipotambulika kama msichana kuwa na matataizo yoyote. Lakini hilo lilibadilika punde tu baada ya kubalehe.
"Niligundua kwamba vitu vyangu vingi ninavyofanya ni vya watoto wa kiume, na kuna wale ambao hawakufarahishwa na hilo hasa watoto wenzangu. Nakumbuka wakiiniita 'huntha'."
Ellie alikuwa ambaye ni mrefu alipenda kucheza mpira wa kikapu pia. Aidha akiwa na miaka 14, aligundua kwamba anavutiwa na wasichana wenzak na hilo likajulikana nawazazi wake.
"Nilikuwa natongoza wasichana na nilifurahia hilo, anasema.
Kisha Ellie akamwabia dadake kwamba yeye ni msagaji.
Lakini akiwa na miaka 15, Ellie aliamini kwamba kuwa mwanamke kunaweza kumfanya kuwa na machaguo machace mno maishani.
Kwa Nele pia, kuwa mwanamke haikuwa jambo la kufurahisha.
"Lilianza nilipobalehe nikiwa na umri wa miaka 9 - na nikaanza kuota matiti kabla hata hajajua kubalehe kun amaanisha nini. Mama yangu alinikataza kwenda nje nikiwa kufua wazi. Tulikuwa tunagombana sana wasababu kila saa nilikuwa ninamuuliza kwa nini kaka yangu anaruhusiwa kwenda nje kifua wazi. Bila shaka mama yangu alitaka kunilinda lakini wakati huo sikuwa ninamuelewa."
Nele akiendelea kukua, wanaume walianza kumtongoza.
Nele as a teenager, a trans man, and todayHaki miliki ya pichaNELE
Image captionNele akiwa amebalehe, kisha akabadilisha jinsia na jinsi alivyo hii leo
Mwili wake ulivyokuwa unakuwa kwa haraka, Nele alijiona mkubwa naikafika wakati akaanza kukataa kula.
Nele alivutiwa na wanawake lakini fikra za kwamba ae magaji ailianza kumtia hofu.
"Nilikuwa nikifikiria kwamba nitakuwa mwanamke muovu, na rafiki zangu hawengetaka kuniona tena kwasababu wangefikiia kwamba nitawageukia."
Akiwa na miwaka 19, Nele alijitokeza kama mtu anayevutiwa na jinsia zote mbili kwasababu hilo lililonekana kuwa salama zaidi kwake.
Nele akaanza kufikiria kuhusu kuondoa matiti yake na kubaini kwamba hilo linawezekana kwa watu waliobadili jinsia zao.
"Nilifurahi sana, lakini mimi sijabadilisha jinsia. Kisha nikaanza kujiuliza je naweza kujifanya kwamba nimebadilisha jinsia? Nikawa nafanya utafiti na ninagundua kwamba mengi yanayosemwa na waliobadilishwa jinsia yanfanana na vile ninavyohisi. Sikuwa naupenda mwili wangu na tangu nilipokuwa mtoto nilitaka sana kuwa kijana."
Ellie and Nele
"Nikaanza kufikiria kwamba sina haja ya kujifanya kuwa nimebadilisha jinsia bali naweza kuibadlisha hasa."
Nele alikuwa anaona machaguo mawili tu kwake yeye - kubadilisha jinsia au kujiua. Baada ya kuwasiliana na shirika lenye kuhamasisha ubadilishaji wa jinsia akatumwa kwa daktari.
"Nilipofika tu, nikaanza kumwambia kwamba nahisi mimi ni miongoni mwa wanaobadilisha jinsia. na moja kwa moja akanishauri nianze kutumia kiwakilishi cha mwanamume. Kisha akaendelea kwamba ni wazi kuwa mimi nataka kubadilisha jinsia na hilo hana mashaka nalo kabisa."
Ndani ya miezi mitatu Nele akaanza kutumia homoni za testosteroni.
Ellie kwa upande wake pia nae alianza kutumia homoni hizo kiume akiwa na miaka 16.
"Niliangalia video kwenye Youtube na nikaona watu waliobadilisha jinsia wanaotumia homoni za testosteroni wamebadilika kutoka kuwa wasagaji hadi wanaume wanopendeza na nikata kuwa na mwili kama wao."
Lakini kwasababu alikuwa mtoto, idhni kutoka kwa wazazi iikuwa muhimu. Wakati anamuona daktari wa kwanza akiwa na wazazi wake walimuambia kwamba asubiri kidogo lakini baada ya kukutana na daktari wa pili, akamridhia ombi lake la kubadili jinsia.
"Aliwaambia wazazi wangu kwamba mabadiliko yote baada ya kubadilisha jinsia yanaweza kubadilishwa tena lakini huo ulikuwa uwongo mtupu. Nilikuwa nimefanya utafiti wangu na nikajua kwamba daktari huyu anadanganya. hata hivyo nilifurahi sana baada ya kusikia amesema hivyo kwasababu hapo ndipo wazazi wake waliporidhia ombi langu."
Eric and Ellie
Eric na mama yake Ellie walikuwa na wasiwasi kuchanganyikiwa katika suala zima la kubadilisha jinsia.
Mara ya kwanza, homoni za testosteroni zilimuathiri Ellie kihisia. Akiwa na miaka 17, alifanyiwa upasuaji wa matiti mara mbili. Na baadaye, alimaliza shule ya upili na kujiunga na chuo kikuu nchini Ujerumani.
Kama mwanafunzi mpya na aliyebadilisha jinsia nchini Ujerumani, Ellie alifikiria kwamba hilo ni jambo ambalo lilikuwa limepitwa na wakati na akawa anaendelea na maisha.
Ellie as a manHaki miliki ya pichaELLIE
Hata hivyo alianza kuwa na hisia tofauti.
"Nilianza kuhisi kwamba kuna mengi ya maisha yangu ambayo ninastahili kuyaficha na sikuwa kuzungumza kwamba nikiwa mtoto nilikuwa msichana."
Ellie and NeleHaki miliki ya pichaNELE
Baada ya muda, Ellie na Nele walikutana na kuwa wapenzi na wakaanza majadiliano ya kina kuhusu jinsia zao.
Na hilo lilitokea baada ya kugundulika kwamba wote uke wao una tatizo la kuwa na ukavu, kuta za uke ni nyembamba mno na pia unavuimbe tataizo ambalo mara nyingi huathiri wanawake ambao wamekomahedhi ambalo pia linatokana na utumiaji wa homoni za testosteroni. Tiba ikawa ni kuanza kutumia tena dawa.
"Lakini haikusaidia zana,"Nele anasema. " Na nikaanza kufikiria kwamba mwili wangu unatumia dawa nyingi za homoni ilihali unaweza kutengeneza homoni zake."
Ellie alihisi vivyo hivyo.
Ellie on the train
Hapo ndipo walipoacha kutumia homoni za kiume za testosteroni lakini uamuzi wa kurejea tena katika jinsia zao za awali yaani kuwa tena wanawake ulikuwa unatia hofu.
"Niliogopa sana hatua ya kuacha kutumia homoni za kiume na urejesha mwili wangu halisi. Hata sikujua ulikuwa unafanana vipi kwasababu nilianza kutumia homoni za kiume mapema sama," Ellie anasema.
"Fikra za kurejea tena kuwa mwanamke zilikuwa zinatia hofu kwasababu kilichonifanya kubadili jinsia ni kukwepa chanagmoto nilizokuwa napitia na kurejea katika jinsia yangu ya awali kunamaanisha kwamba nikurejea tena katika matatizo nililio kuwa nayo. , "Nele anasema.
Ellie na Nele wote hakuna anayepinga haki ya wanaotaka kubadilisha jinsia zao. hata hivyo wana maswali kuhusu ikiwa kubadilihsa jinsia ni suluhu muafaka.

Post a Comment

0 Comments