Kenya: Twiga weupe wa kipekee wameuawa eneo la Kaskazini

Twiga weupe katika hifadhi ya Ishaqbini Hirola kaunti ya Garissa KenyaHaki miliki ya pichaISHQBINI HIROLA CONSERVANCY
Image captionTwiga weupe katika hifadhi ya Ishaqbini Hirola kaunti ya Garissa Kenya
Hifadhi ya wanyama Kaskazini mashariki mwa Kenya imethibitisha kuwa twiga wawili wameuawa ambao ni jamii ya spishi ya kipekee.
Idara ya huduma za wanyamapori nchini Kenya imethibitisha kuuawa kwa twiga hao weupe ikisema kuwa inachunguza mifupa inayoamini kuwa ni ya wanyama hao.
Usimamizi wa hifadhi ambayo twiga hao walionekana kwa mara ya mwisho unaamini kwamba wawindaji haramu ndo waliohusika kwa mauaji ya twiga hao.
Twiga weupe waliouawa walionekana mara ya mwisho kaunti ya Garissa miezi mitatu iliyopita.
Jumanne, msimamizi wa hifadhi ya wanyama ya Ishaqbini Hirola ameiambia BBC kwamba waliokuwa wakiwatafuta wamepata mabaki ya twiga mama na mwanae katika kijiji kimoja.
Baada ya kisa hicho, sasa kumesalia twiga dume mmoja tu mweupe nchini kenya.
Twiga weupe KenyaHaki miliki ya pichaHIROLA COMMUNITY CONSERVANCY
Image captionTwiga weupe Kenya katika hifadhi ya Ishaqbini Hirola
Huku wasimamizi wa hifadhi ya wanyama husika wakiamini kwamba wawindaji haramu ndio waliosababisha mauaji ya twiga hao, kwenye mitandao ya kijamii kumezuka gumzo kwamba huenda chanzo cha kuuawa kwao ni ugomvi unaotakana na pesa za hifadhi hiyo.
Shirika la wanyamapori Kenya limesema linachunguza vifo hivyo.
Twiga weupe walianza kugonga vichwa vya habari kwa mara ya kwanza miaka mitatu iliyopita pale wawindaji haramu walipowabaini, na video ikasambaa kwenye mtandao wa Youtube.
Wanasayansi wanasema hali yao ya kuwa kama chotara kunasababisha seli za ngozi yao kutokuwa na rangi.
Hali hiyo ni tofauti na hali ya kuwa albino kwasababu wanyama huendelea kuwa na rangi nyeusi katika tishu zao laini na kuelezea kwanini twiga hao wana macho meusi.
Hili ni pigo jingine katika juhudi za uhifadhi wa wanyama nchini Kenya.
Mwaka jana vifaru 10 weusi wa kipekee walikufa kwasababu ya sumu ya chumvi wakati wa zoezi la kuwahamisha.

Post a Comment

0 Comments