Tanzania imeripoti kuongezeka kwa visa viwili zaidi vya maambukizi ya virusi vya corona, huku Shirika la afya duniani likilionya bara la Afrika kujiandaa kwa hali mbaya zaidi ya virusi hivyo.
Kuongezeka kwa visa viwili kunaifanya Tanzania kuwa na idadi ya visa vya coronavirus vitano baada ya visa vingine vitatu kutangazwa mapema wiki hii.
Taarifa kutoka wizara ya afya inasema ku wanaoishi jijini Dar es Salaam.
Mgonjwa wa kwanza alisafiri katika mataifa ya Uswiss, Denmark na Ufaransa kati ya tarehe 5 na 13 Machi na kurejea nchini tarehe 14 Machi 2020.
Mwanaume wa pili alisafiri nchini Afrika akusini baina ya tarehe 14 na 16 Machi na kurudi nchini Tanzaniatarehe 17 Machi 2020.
Kwamujibu wa Wizara ya afya wanaoume hao wote wawili wametengwa.
Unaweza pia kusoma:
- Je juhudi za kutafuta chanjo ya coronavirus zimefika wapi?
- Coronavirus: Kwa nini ni hatari kugusa uso wako
- Majibu ya maswali 10 yanayoulizwa sana kuhusu coronavirus
Maafisa wanashughulika kuwatambua watu wengine 46 mjini Arusha, Kaskazini mwa Tanzania na wengine 66 walioko Dar es Salaam wanaoaminiwa kutangamana na wagonjwa wa coronavirus.
Awali Waziri wa afya Ummy Mwalimu alisema kuwa serikali inashirikiana na shirika la afya duniani-WHO na wadau katika kuendelea kutekeleza mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huu".
Raia wametakiwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kadri wanavyopokea taarifa na elimu za mara kwa mara kwa njia mbalimbali.
Katika hatua ya hivi punde ya kukabiliana na mlipuko wa coronavirus Serikali imetangaza kupiga marufuku kuwatembelea wafungwa.
Afrika inapaswa kuamka
Hayo yanajiri huku Barani Afrika kukiwa na jumla ya ujumla vifo 16 vilivyoripotiwa : Sita nchini Misri, sita nchini Algeria, wawili Morocco, mmoja Sudan na mmja wa Burkina Faso.
Afrika walau ni bara lililoathirika kwa kiwango cha chini likilinganishwa na mabara mengine, lakini wataalamu wa afya wanaonya kuwa mifumo duni ya afya ya umma inaweza kuzidiwa uwezo haraka.
Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ananukuliwa na shirika la habari la AFP akisema , "Afrika inapaswa kuamka... katika nchi nyingine, tumeona jinsi virusi vikiongezeka kwa kasi baada ya kugundulika kwa kisa kimoja ."
Burkina Faso alitangaza kifo chake cha kwanza kiliwa ni cha kwanza kutokea kusini mwa jagwa la sahara barani Afrika siku ya Jumatatu - mwanamke mwenye umri wa miaka aliyekua na ugonjwa kisukari.
Maafis anchini humo wanasema mgonjwa alikua ni Rose Marie Compaoré, makamu wa rais katika bunge la taifa.
Nchini Afrika Ksuin, visa vilivyorekodiwa viliongezeka kwa kiwango kikubwa na kufiia 116 siku ya Jumatano, vingi kati yake vikiwahusisha watu ambao wamekua Ulaya.
Idadi hiyo inahusisha maambukizi ya ndani ya nchi ya watu 14.
0 Comments