Korea Kusini, Uchina,China na Singapore ni miongoni nchi za Asia yanayokabiliwa na wimbi la coronavirus, linalosababishwa na watu wanaoingia kutoka nje ya nchi.
China ambako kisa cha kwanza kilitokea,iliripoti kutokuwa na kisa cha coronavirusi siku ya Alhamisi kwa mara ya kwanza tangu mlipuko ulipoanza, yakiwa ni mafanikio makubwa.
Lakini iliripoti visa 34 miongoni mwa watu waliorejea China kutoka nje ya nchi hiyo.
Singapore pia iliripoti visa vipya 47 ambapo 33 kati ya visa vivyo vilikua ni vya wakazi wa Singapore waliojrejea nchi mwao.
Korea Kusini ilishuhudia kuongezeka kwa haraka kwa visa vipya siku ya Alhamisi vikifikia hadi 152, ingawa haijabainika wazi ni vingapi vililiingia kutoka nje ya nchi.
Katika tukio jingine katika kitovu cha maambukizi katika nyumba ya wazee mjini Daegu, watu 74 walipatikana virusi vya corona where 74.
Unaweza pia kusoma:
- Kila kitu unachohitaji kufahamu kuhusu coronavirus
- Majibu ya maswali 10 yanayoulizwa sana kuhusu coronavirus
- Coronavirus: Kwa nini ni hatari kukugusa uso wako
- Jinsi coronavirus inavyoisaidia filamu ya zamani kutazamwa sasa
Japani iliripoti visa vingine vipya vitatu Jumatano. Lakini Hokkaido, jimbo ambalo limeathirika zaidi nchini humo likiwa na visa 154, limeondoa hali ya tahadhari tangu mwishoni mwa mwezi wa Februari,baada ya maafisa kusema kuwa virusi hivyo havisambai tena.
Maafisa wamewataka watu kuendelea kuwa waangalifu na kubaki majumbani mwao, lakini wanasema "hakuna watu wanaoambukizwa virusi ambavyo vimesababisha kuathirika kwa mazingira ya tiba.''
"Tumechukua hatua kubwa zinazozuwia watu kwenda nje, lakini kuanzia sasa, tutaingia katika awamu ya kuzuwia hatari ya kuenea kwa maambukizi huku wakiendelea na shughuli za kijamii na kiuchumi," alisema gavana Naomichi Suzuki Jumatano.
Unaweza pia kutazama:
Tume ya afya nchini Uchina (NHC) iliripoti kuwa hakuna kisa cha maambukizi yaliyofanyika ndani ya nchi nchini China kwa mara ya kwanza tangu virusi vilipoibuka mwishoni mwa mwezi wa Disemba mwaka jana.
Pia ilisema hakuna kisa chochote cha coronavirusi kabisa katika Wuhan, ambacho ni kitovu cha mlipuko-mji ambao awali ulisitisha shughuli zote na watu kukaa majumbani mwao, lakini watu 34 waliwasili kutoka nje ya nchi na kuingiza virusi vya corona nchini humo.
Idadi ya vifo nchini Uchina sasa imefikia watu 3,245, hata hivyo kuna maswali ambayo yamekua yakiendelea kuitokeza juu ya uaminifu wa data zinazotolewa na China.
Nchi zote nne zimekua zikionyesha mafanikio katika udhibiti wa kueneo kwa maambukizi hayo, lakini hofu ya maambukizi iliyoko kwenye maeneo mengine inaweza kukwamisha mafanikio.
Korea Kusini imekua ikisifiwa kwa juhudi zake za ilivyoshughulikia janga, ambazo zimekua zikijumuisha kuyatafuta maambukizi, kuwafanyia vipimo watu wengi na kuwatenga haraka wagonjwa.
Kasi ya maambukizi mapya ya kila siku imepungua tangu mlipuko ulipoingia nchini humo mapema mwezi huu.
Kabla ya Jumatano, idadi ya watu walioambukizwa virusi imekua mara dufu kwa siku nne zilizopita.
Maafisa wa afya wameonya kuwa hakuna muda wa kulegeza mashartii na kwa mara nyingine tena wameutaka umma kuwa mabali na mikusanyiko mikubwa ya watuyakiwemo makanisa, nyumba za wazee, intaneti cafe na kumbi za densi.
'Baki nyumbani, tafadhali '
Kwa sasa wasi wasi si kwa mataifa ya Ulaya na Marekani, bali kiwango kipya kilichoashiriwa cha mlipuko wa virusi vinavyoingia barani Asia kutoka maeneo ya mbali ya bara hilo
Ofisi ya ngazi ya juu ya afya nchini Malaysia JUmatano iliwaomba watu "kaeni majumbani mwenu na ujilinde binafsi na familia yako. Tafadhali".
Malaysia, ambayo imefunga baadhi ya shughuli zake kukabiliana na mlipuko, imekua na visa 710, idadi ambayo ni mbaya zaidi katika eneo la Kusini mashariki mwa Asia.
Vingi kati ya visa vinauhuiano na tukio moja la kidini katika mji mkuu, Kuala Lumpur, la mwezi Februari.
"Tuna fursa ndogo sana ya kuvunja mzunguko wa maambukizi ya COVID-19 ,"Noor Hisham Abdullah, mkurugenzi mkuu wa Afya nchini Malasyia, alisema katika mtandapo wa Facebook.
"Kufeli sio chaguo hapa.Lasivyo tunaweza kukabiliana na wimbio la tatu la virusi hivi, ambao ni mkubwa kuliko tsunami, tukiwa na mtizamo wa 'kwani nini '
Kwa mujibu wa idadi iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani, kuna visa 215,955 vya coronavirus na vifo vilivyotokana na maambukiz hayo ni 8,749 kote duniani.
Shirika la afya duniani (WHO) inasema wengi miongoni mwa - 80% - ya visa hivyo vimetokea Ulaya na kanda ya Pasifiki Magharibi, ambayo inajumuisha sehemu kubwa ya Asia.
0 Comments