Coronavirus: Njia tano za kufanya kazi kutoka nyumbani

Mwanamke akifanya kazi zake nyumbaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamke akifanya kazi zake nyumbani
Maelfu ya watu huenda wakafanya kazi kutokea nyumbani kwa mara ya kwanza wiki hii kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. Kwa wengine ni kama siku nyingine tu.
Takribani watu milioni 1.5 wanafanyia kazi nyumbani, na kwa sasa mpango huo umekuwa maarufu.
Hivyo basi kama hujajitenga, na umeambiwa ufanye kazi ukiwa nje ya eneo la kazi, ni kwa namna gani utabaki kuwa mwenye ufanisi na kuendeleza bidii ya kazi?

1. Vaa nguo

Kwa baadhi ya watu, hali ya kuwa umevaa nguo za kulalia siku nzima ni kitu kinachosukuma hamu ya kufanya kazi kutokea nyumbani. Lakini kuoga na kuvaa nguo hakutasaidia kuchangamsha akili yako pekee, lakini pia kisaikolojia itakupa msukumo wa kujiandaa kuanza kufanya kazi.
Kwa kutegemea na aina ya kazi yako, Baadhi ya watu wanaona kuvaa mavazi rasmi ya kazi wakiwa nyumbani inasaidia, hasa kama wanataka kupiga simu za kikazi za video.
Kuvaa mavazi ya heshima wakati wa kufanya kazi za ofisini ukiwa nyumbani kunainua ari ya kutoka nyumbani, kubadili muonekano kwa kubadili nguo za kazi kunasaidia kuufanya ubongo kuelewa kuwa siku ya kazi imekwisha.

2. Kuweka mipaka

Ikiwa umeajiriwa na kampuni, ni wazi umeweka saa kadhaa za kufanya kazi, na ni muhimu kuzingatia hilo ikiwa utakuwa unafanya kazi kutokea nyumbani. Kuwa tayari kuanza siku yako muda ule ule kama utakaokuwa umewasili ofisini au mahali pako pa kazi na maliza siku yako muda uleule unaokuwa mahali pako pa kazi.
Mwanablogu, Em Sheldon na mwandishi wa kujitegemea, anasema yeye hufuata ratiba hiyo hiyo hata akifanyia kazi nyumbani. Anashauri '' kulala kwa muda unaofaa ili upate usingizi wa kutosha kwa ajili ya kuamka kwa muda unaofaa siku inayofuata.
Unapofanya kazi nyumbani , ni vyema kubaki kwenye ratiba kama ile unayofanya kazi ofisiniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUnapofanya kazi nyumbani , ni vyema kubaki kwenye ratiba kama ile unayofanya kazi ofisini
"Pia mimi hufanya mazoezi hii inamaanisha lazima niamke na kwenda," anasema. "Mara tu unapofanya jambo tena na tena, inakuwa tabia, kwa hivyo wiki ya kwanza inaweza kuwa changamoto lakini mwishowe inakuwa sehemu ya utaratibu wako."
Mwisho wa siku ya kufanya kazi, ni bora kuzima kompyuta yako na kuondoa karatasi na vitu vingine. Nafasi inayoruhusu, tenga eneo maalum, tofauti katika nyumba yako ambapo unaweza kujiwekea dawati sawa na eneo lako la kazi.
A Twitter user shares some tips for working from homeHaki miliki ya pichaTWITTER
Kama kuna watu wengine nyumbani, kutafuta nafasi ambayo si rahisi kusumbuliwa ni muhimu, kama alivyobaini Profesa Robert Kelly mwaka 2017. alikuwa akihojiwa moja kwa moja na BBC,akaeleza namna watoto wake walipokuwa wakiingia kwenye chumba lichokuwa akifanyia kazi.
3. Toka nje utembee (kama haujajiweka karantini)
Kufanya kazi nyumbani haimaanishi kuwa ujifungia nyumbani siku nzima, si vibaya kutoka ndani ya nyumba angalau mara moja kwa siku.
Hivyo vaa viatu yako, toka nje na furahia hewa safi. Hali hii itasaidia kukupa mawazo mapya au namna nyingine ya kushughulikia jambo lililokuwa likikupa ugumu.
Mwanamke akiwa matembeziniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamke akiwa matembezini
Matthew Knight, mwanzilishi wa Leapers, kikundi ambacho kinasaidia watu wanaojiajiri na wafanyikazi wa mkataba wa muda mfupi, anasema kutoka nje kitu cha kwanza kunamsaidia kuhisi kama ni wakati wa kufanya kazi.
"Kuna suala la akili kwa kila mtu ambayo inakufanya uhisi kana unafanya kazi," anasema. "Nitaondoka nyumbani na kuzunguka na nahisi kama hivi sasa niko kazini. Tafuta njia za kujiweka kwenye mipaka hiyo vinginevyo inakuwa ngumu kuzoea."
Ikiwa huwezi kwenda nje, unaweza hata kuleta mazingira ya ofisi nyumbani kwako.
"Ninapenda sana na kuwa karibu na watu, kwa hivyo mimi hutumia sauti kusaidia kutengeneza mazingira," anasema Gillian Roche-Saunders, ambaye kampuni yake yote ya ushauri inafanya kazi nje ya ofisi.
Yeye hutumia programu inayotoa sauti za nyuma kama vile gari moshi au mazungumzo kwenye mgahawa wa kahawa.
4. Pokea simu
Kama unafanya kazi kutokea nyumbani, kuna uwezekano kuwa utakuwa peke yako, hivyo hautasumbuliwa na wafanyakazi wenzako' mazungumzo au kelele nyingine za ofisi.
Unapokuwa kazini, kuna uwezekano wa kuwa na mazungmzo na wenzako lakini ukifanya kazi kutokea nyumbani, utatumia siku nzima bila kuzungumza na mtu yeyote hali inayoweza kuwa kama kujitenga.
Ni vizuri ukafanya pia mawasiliano ya simu kuliko ya barua pepeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNi vizuri ukafanya pia mawasiliano ya simu kuliko ya barua pepe
Pata muda wa kupokea simu na uwe na mazungumzo, kuliko kutegemea barua pepe au ujumbe wa papo kwa hapo.
''Watu wengi zaidi hujificha kwenye barua pepe kuliko kushika simu na kuzungumza na wafanyakazi wenzake,'' anasema Hugo Mortimer-Harvey ambaye amekuwa akifanya kazi kutoka Uhispania kama mshauri wa mahusiano ya umma tangu mwaka 2018.
''Wakati ukitumia siku nzima kufanya kazi mwenyewe, kuwapigia watu na kuwa na mazungumzo kunaweza kutoa msukumo na pia kufanya kazi zako vizuri kuliko mfululizo wa barua pepe.''
A Twitter user shares some tips for working from homeHaki miliki ya pichaTWITTER
5. Jipumzishe mara kadhaa
Ni vizuri kuwa na utaratibu unapofanya kazi kutokea nyumbani kupumzika, isiwe kung'ang'ania kufanya kazi mfululizo.
Na usigande kwenye kompyuta yako siku nzima. Ni muhimu kujipumzisha kidogo kuyaondoa macho yako kutoka kwenye kioo cha kompyuta na kunyanyuka kutoka kwenye kiti chako na kutembea tembea kidogo kama ambavyo ungefanya ofisini.
Mwanamke akijipa mapumziko kwa kujinyoosha viungoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamke akijipa mapumziko kwa kujinyoosha viungo
Utafiti pia umebaini kuwa mapumziko mafupi mafupi siku nzima yana faida kuliko kuwa na mapumziko marefu baada ya muda mrefu.
Ellie Wilson ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Virtalent, yenye wafanyakazi zaidi ya 50 wanaofanya kazi wakiwa nyumbani.
''Ni muhimu kunyanyuka na kujinyoosha, kutembea tembea hata kutoka nje na kutembea kujipumzisha na kazi za kwenye kompyuta yako,'' anaeleza.
''Kuzama kwenye kazi bila kupumzika kunamaanisha kuwa kiwango cha ufanisi kinashuka, unakuwa mchovu zaidi na usiye na msukumo na nguvu ya kumaliza unachokifanyia kazi.

Post a Comment

0 Comments