Coronavirus: Mwanamuziki wa Bongo Flava nchini Tanzania athibitisha kuwa na maambukizi ya virusi

Hamisi Mwijuma (Mwana FA)Haki miliki ya pichaMWANA FA- INSTAGRAM
Image captionHali ya mwanamuziki wa Bongo Flava imeimarika
Mwanamuziki wa Bongo Flava nchini Tanzania, Hamisi Mwijuma, maarufu Mwana FA ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa amegundulika kuwa ameathirika na virusi vya COVID- 19 au corona.
FA amesema alifanya vipimo hapo jana na kupatiwa majibu yake hii leo vilivyobainisha kuwa ameathirika na virusi hivyo.
Katika kipande chake cha video alichokiweka kwenye mtandao huo, Mwana FA alieleza kwenye ukurasa wake kuwa alitoka Afrika Kusini juzi na kubaini kuwa joto lake la mwili halikuwa la kawaida.
''Sababu ya kufanya hivyo nilikuwa natoka safarini Afrika Kusini, joto langu la mwili lilikuwa halieleweki, linapanda, linashuka hivyo nilivyorudi kwa sababu habari duniani inayofahamika ni hiyo nikawa nimejitenga ili kuhakikisha siwaathiri watu wengine''.
Mwanamuziki huyo amesema kwa sasa ile homa aliyokuwa akiihisi juzi kwa sasa haipo tena lakini bado amejitenga wakati afya yake ikiendelea kuimarika.
Hapo awali Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Sallam SK naye alithibitisha kuwa amekutwa na virusi vya corona na sasa yupo chini ya uangalizi na afya yake inaendelea vizuri.
Jinsi ya kuepuka maambukizi
Jinsi ya kuwa salama
Image captionJinsi ya kuwa salama


Post a Comment

0 Comments