NOAM GALAI
Virusi vinavyoua vya coronavirus sasa vimekumba majimbo yote 50 huku jimbo la West Virginia likiripoti kisa cha kwanza cha maambukizi Jumanne.
Akitangaza kisa cha kwanza cha Covid-19 katika jimbo la West Virginia, Governor Jim amesema kuwa : "Tulifahamu kuwa hii inakuja."
Jiji la New York City limesema linaangalia uwezekano wa kufunga shughuli zote za umma sawa na ile iliyowekwa katika eneo la San Francisco Bay.
- Je madai ya Trump kuhusu coronavirus Marekani ni ya kweli?
- Mtu wa kwanza ajitolea kufanyiwa chanjo ya coronavirus
- Imani sita potofu kuhusu maambukizi ya virusi vya corona
Kumekua na vifo 108 nchini Marekani vilivyotokana na coronavirus na zaidi ya visa 6,300 vimethibitishwa kote nchini Marekani.
Kumekua na takriban visa 200,000 kote duniani na karibu watu 8,000 wamekufa kutokana na virusi vya corona.
Huku utawala wa rais Trump ukiangalia jinsi ya kutoa pesa za kuchochea ukuaji wa uchumi zilizoripotiwa kuwa sawa na dola zipatazo bilioni $850, waziri wa fedha Steve Mnuchin akisema kuwa utawala "unaangalia jinsi ya kuwatumia hundi Wamarekani mara moja".
Kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia hadi 20% - kikiwa kimeongezeka mara dufu ikilinganishwa na wakati wa msukosuko mkubwa wa kiuchumi wa mwaka 2008.
GETTY IMAGES
Je Jiji la New York linaangalia uwezekano wa kufanya nini?
Meya Bill de Blasio alisema ataamua katika kipindi cha siku mbili ikiwa atawaagiza wakazi wa jiji hilo wapatao milioni 8.5 "kupata hifadhi shelter in place".
Hatua hiyo inaweza kuwafanya watu wasalie nyumbani kwao tu, huku wakiruhusiwa kufanya matembezi ya lazima kununua bidhaa za nyumbani au dawa,kutembeza mbwa au kufanya mazoezi ili mradi waepuke mikusanyiko ya umma.
" Ni uamuzi mgumu, mgumu sana vigumu ,"Bwana de Blasio alisema. "Hatujawahi kuwa katika hali hii kabla. Sijawahi kusikia kitu kama hiki katika historia ya jiji la New York ."
Maafisa katika eneo la San Francisco Bay wamekwishatoa amri kwa wakazi milioni 6.7 kubakia nyumbani isipokua inapokua lazima hadi tarehe 7 Aprili.

Unaweza pia kusoma:
- Coronavirus: Kwa nini ni hatari kushika uso wako
- Jinsi mfumo wa kinga unavyoweza kupambana na virusi vya corona
- Majibu ya maswali 10 yanayoulizwa sana kuhusu coronavirus
- Imani sita potofu kuhusu maambukizi ya virusi vya corona

Jeshi la Marekani linaweza kuwa na mchango gani?
Makamu rais wa Marekani Mike Pence amesema kuwa ikulu ya White House huenda ikaliita jeshi la Marekani kuanzisha hospitali katika maeneo yaliyokumbwa na virusi ikiwa wataombwa kufanya hivyo na magavana wa majimbo.
Aliuambia mkutano wa waandishi wa habari wa White House Jumanne kwamba wanajeshi wahandisi wanaweza kuombwa kujenga hospitali, sinazofahamika kama -kikosi cha Mash (hospitali inayozunguka maeneo ya jeshi ) au kuimarisha hospitali zilizopo.
Mkuu wa kikosi cha Mash cha Pentagon Mark Esper amesema kuwa Marekani itasaidia uwepo wa barakoa za kupumulia milioni tano na vifaa vya kupumua hadi 2,000 kuanzisha idara ya afya ya Marekani
Alisema kuwa jeshi litasaidia pia kufungua maambara 14 za kupima virusi vya corona kuwapima raia wa kawaida.
EPA
Ni zipi taarifa za hivi punde kutoka Marekani?
Jumanne, Florida ilijiunga na majimbo 11 katika kufunga baa na migahawa katika moja ya sikukuu maarufu ya St Patrick ambayo Marekani imeiathimisha katika wakati wa amani.
Waandalizi wa Kentucky Derby - ambalo ni tukio la michezo ambalo limekua likiendelea - limeahirisha mashindanoya mbio za farasihadi mwezi Septemba.
Lilikua ni tukio la hivi karibuni lililojipata likiondolewa kutoka kwenye kalenda kwasababu ya coronavirus, sambamba na shindano la gofu la Masters na la Machi la mpira wa kikapu- Madness basketball extravaganza
Rais Trump anashughulikia vipi coronavirus?
Rais Donald Trump - ambaye anataka kuchaguliwa tena mwezi wa Novemba- aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Jumanne mchana kuwa vikwazo vya vya kusafiri ndani ya Marekani vinajadiliwa.
"Unaweza kufunga shughuli zote kitaifa," Bwana Trumpalisema. "Tuna matumaini, tutahitaje hilo. Ni hatua kubwa sana."
Pia alitetea ujumbe wake wa Twitter alioutoa Jumatatu akiyaita maambukuzi "Virusi vya Kichina", ambayo wakosoaji wanasema ni ubaguzi.
"Ilitoka Uchina "aliwaambia maripota.
Bwana Trump alisema kuwa Jumanne kuhusiana na mlipuko : "Nilihisi kuwa ni janga lamuda mrefu kabla ya ktangazwa kuwa janga
Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 18 Machi 2020
Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.
0 Comments