Coronavirus: Je ni hatua gani zimechukuliwa na EU kuzuia maambukizi?

A German police officer controls a motorist at the French-German border between Kehl and StrasbourgHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMpaka wa Ufaransa na Ujerumani unaruhusu bidhaa tu na wanaotembea kwa miguu kupita
Muungano wa Ulaya umepiga marufuku wasafiri kutoka nje ya muungano huo kwa siku 30 katika hatua ambayo haikutarajiwa ya kufunga mika yake kufuatia mzozo wa coronavirus.
Hatua hii inayahusu mataifa 26 wanachama wa EU pamoja na Iceland, Liechtenstein, Norway na Uswiss. Raia wa Uingereza hawataathiriwa na hatua hiyo.
Marufuku hiyo inatolewa huku idadi ya vifo vinavyotokana na mlipuko wa coronavirus ikiendelea kuongezeka katika nchi za Italia, Uhispania na Ufaransa imeweka masharti kali ya kuzuwia shughuli za umma na kuwataka raia wasalie majumbani mwao.
Ulaya imeathirika vibaya na virusi ambavyo vimewauwa watu 7 ,500 duniani.
Wakati huo huo mashindano ya kombe la Euro 2020 limeahirishwa kwa mwaka mmoja.
Virusi vya corona vimewaathiri zaidi ya watu 185,000 kote duniani, kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO).
Je ni hatua gazi zimechukuliwa na EU?

Marufuku ya safari itaathiri raia wote ambao sio wanachama wa EU wanaotembelea nchi za Muungano huo, isipokua wakazi wa muda mrefu, wanafamilia kutoka nchi wanachama wa Muungano huo na wanadiplomasia, wafanyakazi wa mipaka na wahudumu wa afya na watu wanaosafirisha bidhaa.
Kwa kawaida matembezi ya raia kutoka za eneo la Schengen wamekua na uhuru wa kusafiri katika mataifa ya Muungano wa Ulaya bila pingamizi.
Lakini katika siku za hivi karibuni nchi nyingi zimeweka masharti ya kuingia kwenye mipaka yake ili kuzuwia kusambaa

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Hii imeifanya tume ya muungano huo kupendekeza kuwa Muungano huo kuchukua hatua katika mtindo wa pamoja na kuweka masharti ya kuingia katika muungano mzimakutokana na ombi la rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Hatua zilikubaliwa katika kiao kilichofanyika kwa njia ya video baina ya viongozi wa EU siku ya Jumanne mchana na sasa zitatakiwa kuekelezwa na nchi wanachama.
"Walisema watafanya hivyo mara moja ,"alisema Kamishna mkuu wa EU Ursula von der Leyen katika mkutano na waandishi wa habari. "Hili ni jambo zuri, ili tuwe na mbinu ya pamoja ya kushughulikia mipaka''
Uingereza na Jamuhuri ya Ireland - ambayo ni sehemu ya EU lakini ni mwanachama wa Schengen - itakaribishwa kujiunga na hatua hiyo.
Ilikua ni muhimu kwa muungano wa EU " kuwa wazi " kuhusu wkufungwa kwa mipaka ya ndani , Bi Von der Leyen aliesma , kwasababu "watu wengi walikua wamekwama".
Habari zaidi juu ya coronavirus
Je ni zipi taarifa za hivi punde nchini Ulaya juu ya coronavirus?
Nchini Ufaransa, raia wanoondoka majumbani mwao lazima wabebe waraka unaoelezea ni kwa nini, huku nchi hiyo ikiwa imeweka faini ya €135 ($150; £123) kwa yeyote atayekiuka amri ya kutotembea bila sababu.
Rais Emmanuel Macron awali aliwaamuru watu kubaki majumbani mwao na waende nje tu pale wanapoenda kufanya majukumu muhimu. Bwana Macron alisema: "Tuko vitani... hatupambani na jingine lolote lile wala nchi yetu wenyewe. Lakini adui yuko hapa, haonekani, hawezi kuguswa ... na anasonga mbele."
Nchini Uingereza, idadi ya vifo imefikia watu 71, na watu wamekua wakiambiwa waepuke matangamano ya kijamii, watu kufanyakazi nyumbani ikiwa wanaweza na kuepuka safari za kigeni zisizo muhimu.
Waziri Mkuu Bois Johnson Jumatatu aliwataka watu waepuke kwenda kwenye maeneo kama vile baa,vilabu vya pombe na migahawa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisem Ufaransa inapambana na adui asiyeonekana wala kuguswa alipokua akitoa maagizo ya udhibiti wa coronavirus
Image captionRais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisem Ufaransa inapambana na adui asiyeonekana wala kuguswa alipokua akitoa maagizo ya udhibiti wa coronavirus
Wakati huo huo mshauri mkuu wa serikali wa masuala ya kisayansi amesema ''itakua na matokeo mazuri'' kama watu 20,000 au wachache zaidi watakufa kutokana na virusi vya coronavirus nchini Uingereza.
Mazungumzo ya hivi karibuni ya Brexit yamecheleweshwa.
Idadi ya vifo katika nchini ya Uhispania imeongezeka kutoka watu 2,000 hadi 11,178. Mamlaka nchini humo zimeweka marufuku ya matembezi na shughuli zisizo za lazima kwa rais wa nchi hiyo milioni 47.
Italia sasa ni nchi ya pili iliyokumbwa na mlipuko baada ya Uchina. Kumekuwa na masharti makali ya kuzuwia mikusanyiko ya umma ili kujaribu kusitisha usambaaji waq virusi.
Masharti yalitekelezwa kwa mara ya kwanza kaskazini mwa nchi, kabla hayajatekelezwa kitaifa.
Serikali imewataka watu milioni 60 wa Italia kubakia majumbani mwao pale inapowezekana.
Wakazi wanaweza kutoka nje ya nyuma zao tu pale wanapokua na hitaji la dharura, kama vile kununua bidhaa muhimu na wanatarajiwa kutembea na kibali maalum kinachoelezea sababu ya safari yao.
Wanaokiuka amri hiyo wanakabiliwa na tisho la kutozwa faini ya dola 235 kwa kuvunja sheria au hata kufungwa jela kwa muda wa miezi mitatu.

Unaweza pia kutazama:

Coronavirus: Raia wa Italia watiana moyo kwa nyimbo za kizalendo
Ujerumani ambayo ina zaidi ya visa zaidi ya 6,000 na vifo 13, imezuwia ibada za kidini na ikawambia watu wafute safari zao za ndani na nje ya nchi yao au safari za mapumziko y za kitalii
Maeneo kama baa, maeneo ya burudani, michezohifadhi za wanyama na viwanja vya michezo vimefungwa. Shuel pia zimefungwa
Ireland inaweza kuwa na visa 15,000 vya coronavirus kabla ya mwisho wa mwezi Machi, amesema Waziri Mkuu Leo Varadkar. Serikali tayari imekwishafunga maeneo ya burudani, shule na vyuo vikuu.
Hali ilivyo kwingineko:
Saudi Arabia inatangaza faini ya hadi dola $133,000 (£110,000) kwa mtu yeyote atakayeshindwa kutangaza taarifa sahihi za kiafya zinazomuhusu pamoja na maelezo anapoingia nchini.
Badhi ya mataifa yameweka marufuku unapowasili, kufunga mipaka yao ya anga na ardhini.
Virusi vya corona
Wengine wameweka amri ya kuwekwa karantini kwa muda wa siku 14 kwa watu wote wanaosafiri kwa ndege kuingia nchini mwao, mkiwemo amri inayomtaka mtu kujitenga binafsi katika makazi binafsi kama vile kwenye hoteli.
Yeyote ambaye haheshimu sheria mpya nchini Australia atakabiliwa na tisho la faini nzito na hata kifungo cha jela katika baadhi ya maeneo ya nchi. Faini kubwa zaidi iliyowekwa Magharibi mwa Australia ambako wale wanaokiuka amri hiyo wanakabiliwa na kulipa faini ya hadi dola za Australia- A$50,000 (£25,000).
Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameonya kwamba wasafiri wanaoshindwa kuheshimu sheria za kujitenga wanaweza kukabiliwa na faini na kufukuzwa .
"Iwapo utakuja hapa na hauna nia ya kufuata maombi yetu ya kujitenga binafsi,kusema kweli haukaribishwi na unapaswa kutoka nchini kabla hatujakurejesha ulikotoka ,"alisema.
Nchini Marekani , ikilu ya White House inaangalia jinsi ya kutoa pesa za kuchochea uchumi zilizoripotiwa kuwa sawa na dola zipatazo bilioni $850, huku Waziri wa fedha Steve Mnuchin akisema kuwa utawala "unaangalia jinsi ya kuwatumia hundi Wamarekani mara moja".
Jumla ya visa vya coronavirus vimepanda hadi zaidi ya 4,200, ikiwa na huku vifo 75, kimesema kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Marekani. Visa vingi viko New York (669), Washington (708) na California (369),
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Hii imeifanya tume ya muungano huo kupendekeza kuwa Muungano huo kuchukua hatua katika mtindo wa pamoja na kuweka masharti ya kuingia katika muungano mzimakutokana na ombi la rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Hatua zilikubaliwa katika kiao kilichofanyika kwa njia ya video baina ya viongozi wa EU siku ya Jumanne mchana na sasa zitatakiwa kuekelezwa na nchi wanachama.
"Walisema watafanya hivyo mara moja ,"alisema Kamishna mkuu wa EU Ursula von der Leyen katika mkutano na waandishi wa habari. "Hili ni jambo zuri, ili tuwe na mbinu ya pamoja ya kushughulikia mipaka''
Uingereza na Jamuhuri ya Ireland - ambayo ni sehemu ya EU lakini ni mwanachama wa Schengen - itakaribishwa kujiunga na hatua hiyo.
Ilikua ni muhimu kwa muungano wa EU " kuwa wazi " kuhusu wkufungwa kwa mipaka ya ndani , Bi Von der Leyen aliesma , kwasababu "watu wengi walikua wamekwama".
Habari zaidi juu ya coronavirus
Je ni zipi taarifa za hivi punde nchini Ulaya juu ya coronavirus?
Nchini Ufaransa, raia wanoondoka majumbani mwao lazima wabebe waraka unaoelezea ni kwa nini, huku nchi hiyo ikiwa imeweka faini ya €135 ($150; £123) kwa yeyote atayekiuka amri ya kutotembea bila sababu.
Rais Emmanuel Macron awali aliwaamuru watu kubaki majumbani mwao na waende nje tu pale wanapoenda kufanya majukumu muhimu. Bwana Macron alisema: "Tuko vitani... hatupambani na jingine lolote lile wala nchi yetu wenyewe. Lakini adui yuko hapa, haonekani, hawezi kuguswa ... na anasonga mbele."
Nchini Uingereza, idadi ya vifo imefikia watu 71, na watu wamekua wakiambiwa waepuke matangamano ya kijamii, watu kufanyakazi nyumbani ikiwa wanaweza na kuepuka safari za kigeni zisizo muhimu.
Waziri Mkuu Bois Johnson Jumatatu aliwataka watu waepuke kwenda kwenye maeneo kama vile baa,vilabu vya pombe na migahawa.

Post a Comment

0 Comments