MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Freeman Mbowe na wenzake nane kulipa faini ya Shilingi milioni 350 ama kutumikia kutumikia kifungo cha miezi mitano gerezani baada ya Mahakama kuwakuta kila mmoja na hatia katika kesi ya uchochezi yenye mashtaka 12 iliyokuwa inayowakabili.
Hukumu hiyo iliyochukua takribani saa nne imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema upande wa mashtaka unaweza kuthibitisha pasipo kuacha shtaka kuwa washtakiwa wote wametenda makosa yanayowakabili kasoro shtaka la kula njema tu ambalo upande wa mashtaka wameshindwa kuthibitisha.
Katika adhabu hiyo, Mbowe amehukumiwa kulipa Sh.Milioni 70, Halima
Mdee Sh.Milioni 40, Dk.Mashinji kulipa Sh.Milioni 30, John Heche Sh.Milioni 40, Msigwa Sh.Milioni 40, Bulaya Sh.Milioni 40, Mnyika Sh.Milioni
30, Salum Mwalimu Sh.Milioni 30 na Ester Matiko Sh.Milioni 30.
Kwa mujibu wa Hakimu Simba iwapo watashindwa kulipa faini hiyo wataenda jela miezi mitano mitano kwa kila.
0 Comments